Thierry Henry amvuta Jokate Arsenal

Thierry Henry amvuta Jokate Arsenal

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
MSANII wa muziki na mwanamitindo nchini, Jokate Mwegelo, ametangaza kuwa shabiki mpya wa klabu ya Arsenal, baada ya kukutana na mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo na timu ya Taifa ya Ufaransa, Thierry Henry, nchini Afrika Kusini.

Wawili hao wamekutana kwenye mchezo wa kikapu wa NBA Africa Game nchini humo mwishoni mwa wiki iliyopita na kupata chakula cha pamoja.

Jokate alitumia akaunti yake ya Instagram kuposti picha akiwa na mchezaji huyo, kisha kuweka wazi kuwa anahamia klabu hiyo ya Arsenal.


“Furaha kubwa kula chakula na Thierry Henry kabla ya kuanza kwa mchezo wa NBA Africa Game, kuanzia sasa ninahamia rasmi klabu ya Arsenal, naomba ushauri kwa kuwa ninaambiwa kuishabikia timu hiyo unatafuta mawazo,” aliandika Jokate.

upload_2017-8-9_17-51-22.png
 
Mapenzi kwenye jambo lolote hutokea natural kutoka rohoni sio kwasababu ya flani......haiwezekani

Huyo anaigiza tu wala hataweza
 
Kanajiona kazuriii and relevant after all these years. If she's really smart, angeolewa na kuwa na mainstream career inayokubalika instead of seeking constant public attention and cheap popularity on the daily.
 
Jokate ana bahati mbaya kila anapojaribu kujiinua watu wanamzamisha chini zaidi, anataka umaarufu kwa nguvu hajui atoke vipi.
 
Niko Arsenal long nikiwa primary school, pia niko Yanga. Yes kuwa shabiki wa Arsenal yakupasa kuwa mvumilivu japo huwa najipa matumaini siku Wenger akiondoka mambo yatakuwa mule mule.
 
Kweli, hii dunia vituko havitakaa viishe bali vinaongezeka kila kukicha.
 
Huyu sio mchoyo, kama alikubali kumchukua Diamond akiwa mikononi mwa wema ataachacje kumchukua Hendry ambae mkewe hata hamjui?!


Aiseeeeeh,
Hii nchi ya Mwl. Nyerere, ina siri nyingi!
 
Back
Top Bottom