Sasa hicho chake unakulaje "kuganga njaa"?Kuna namna yoyote au style maalum?Na kama kumwambia huwezi kwa woga wa kumwumiza hiyo namna ndio haitomuumiza?
Badala ya kufanya kitu cha kawaida kuelewa kichukue muda kwa kutumia mafumbo just be open. Mwambie mi mboga za majani siwendi zitiwe maji mengi, au sipendi zikaangwe,mchuzi sipendi uwe kama maji ya kunawia mikono mtu atakusoma na atatafuta namna nyingine. Na sijui akiumia, well she'll get over it. Uncle wangu alimwambiaga mke wake wazi kabisa kwamba "mpenzi unaniabisha" maana alipika ndizi kajaza maji utadhani kahamishia mto jikoni wakati wa upenzi hata sio uchumba wao. Sasa hivi wako ndani ya ndoa na wana furaha. Kwahiyo hao unaowaita 'smart' labda kama sio WAELEWA nna uhakika wanaweza wakakulewa ukiwaambia maana wakati mwingine watu hukazana kufanya kitu kwa kudhani we unafurahia kwabsababu hujasema otherwise na sio hujaonyesha otherwise.