Wakuu Konte na Ntamb,
Binafisi nakubalina nanyi kwa 100%. Ni dhairi kuwa vyama vingi vizivyo vya kiserikali vimekuwa na mwelekeo wa kimaslahi zaidi kuliko kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake. Hii inechangia sana raia wengi kupoteza imani na hivyo vyama hasa pale inapofika katika kuvihusisha kutatua matatzio ya wananchi. Kwa mfano, zamani kulikuwa na watu binafsi wanaojitolea kusaidia moja kwa moja kutoa ushauri na pia kuanzisha halakaki za kuibua hoja ambazo ziliifanya Serikali iamke na kuona uwepo wa dosari katika utendaji wake. Watu wa jinsi hii walifanyakazi kwa kujitolea kupitia mashirika hayo yasiyo ya Kiserikali au kwa binafsi zao. Kwa mfano kama akina Tundu Lissu na Rugemeleza Nshala wao binafis au kupitia Lawyers' Environmental Action Team (LEAT) katika sakata la Mradi wa Bulyanhulu.
Nakubaliana nanyi 100% kuwa fedha za umma ambazo zinatengwa katika bajeti za Serikali kila mwaka zinapotea kutokana na kukosekana kwa uadilifu na mfumo wa kuwafanya watendaji katika Sekta ya umma wawe waadilifu (accountability of Government to its people). Ni dhairi kuwa uwepo wa "Think Tank" zenye nguvu kunaweza kuifanya Serikali yetu iweze kutimiza mema kwa wananchi wake kwa kupitia uibuiaji wa hoja na kuzifuatilia kwa kina mapka mwisho. Tumeona jinsi ambavyo nchi za wenzetu, Mashirika yasiyo ya Kiserikali yalivyo na nguvu na sauti ya kuweze "kuhamisha Milima na kufukia mabonde". NGOs hizi au watu binafsi wameweza kuzifanya Serikali zao ziwe makini katika kila jambo na hata kuwajibika kwa watumishi wa umma pale mambo yanapokwenda kinyume na matarajio iwe kwa kutumia dhamana kwa maslahi binafsi au kwa Uzembe, kila senti inamwajibisha kiongozi.
Wengi walitarajia uwepo wa vyama vingi vya siasa (Political Parties) na vyama visivyo vya kiserikali (NGO) Tanzania kunaweza kusaidia mabadiliko na wanachi wakayaona hayo. Lakini hakina ukifuatilia kwa undani utaona jinsi siku zinavyosonga, biashara ya vyama hivi imekuwa ni porojo na ushindani wa kutafuta mazingira "mema ya ulaji tupu" (uongozi na maslahi binafsi) kuliko watu wao yaani watanzania. Vingi ya hivyo vyama havina mwamko, wasomi wengi wanaibuka kila kukicha lakini hawapendi kutumia muda na elimu zao kwa faida ya Taifa kama walivyofanya wenzetu huko nyuma mpaka leo nchi hii ikawa huru.
Wasomi wengi hawapendi kushiriki katika tafiti za kuibua hoja za msingi, wengi hawapendi kuandika wala kusoma..wengi wamekuwa wakitumika au kutumikishwa kwa maslahi ya mfumo tulionao wa kunufaisha wachache badala ya kujitumikisha kwa maendeleo ya walio wengi. Tunaibua tabaka la utengano mkuu, wa walionazo na wasio nazo...wenye nguvu na wasio na nguvu..
Kama nikiangalia tafakairi ya Mzee Konte, waweza kuona pia hata hiyo sekta ya Kilimo ndio imekuwa ikitumika zaidi ya miaka kumi iliyopita kuhamishia na kufichia rasilimali nyingi (fedha za umma) ambazo hazina matokeo kwa walengwa. Bajeti za kisekta zimekuwa zikiongezeka kwa silimia kadhaa mwaka hadi mwaka, wabunge wetu na wasomi hawana muda hata wa kupima matokeo ya ongezeko la bajeti na utekelezaji kwa vitendo wa yale yaliyodhamiriwa katika bajeti husika ( kwa mfano, ukifuatilia mfumo wa mijadala Bungeni, waheshimiwa wakiambiwa Serikali imenunua matrekta kadhaa, hoja inakuwa imefungwa bila hata kuuliza wala kutaka kuona yapo wapi na yanafanya nini na yameongeza tija kwa kiasi gani kutokana na kuwepo kwake sambamba na uwepo wa rasilimali nyingine zinazoigharimu fedha za Umma kama Ruzuku za Pembejeo, Wataalamu wa Kilimo, Miradi ya Maendeleo nk)...
Hizo kauli mbiu kama "KILIMO KWANZA" sasa imekuwa wimbo wa siasa..na walioibua unaweza kuona ni "wafanyabiashara" ambao kimsinigi hata hicho kilimo kwao ni wimbo wa zamani. Zitihada zilizofanyika kuleta Kauli Mbiu ya KILIMO KWANZA ni kuunganisha Sera na Mikakati ilivypo tu lakini ikija kwenye utekelezaji wake, hakika hata baadhi ya wakuu wetu wa nchi hawajui tutokako wala tuendako (kwa wale mliofuatilia kongamano la "WEF" lililofanyika miezi michache iliyopita - Dar es Salaam, mliweza kujionea jinsi ambavyo hata Mhe. Rais alivyoshindwa kabisa kuelezea kwa kina mikakati ya kimaendeleo katika Sekta ya kilimo nchini sambamba na dhana ya "KILIMO KWANZA".
Hakuna anayeweza kubainisha kwa nini Kilimo kina kufa pamoja na historia ya miradi ya wafadhiri mingine ambayo ipo na imewahi kuwepo kuwalengwa kwa watu hao hao (wakulima))!!!!.
Sasa kuna Jitu kuu linaitwa "THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETIES" hiki chombo kilianzishwa takribani miaka saba iliyopita kikiwa na malengo makuu ya kusaidia jitihada za Serikali katika kuwakwamua wananchi kijamii na kiuchumi ikiwemo kuwafanya wananchi wajue haki zako na kujitambua, na kujiletea maendeleo kupitia Sera na Mikakati iliypo kama Tanzania Development Vision (TDV -2025); MKUKUTA nk.
Kwa muda sasa kupitia vyombo vya habari, hiki chombo kimeonekana kikiibua mijadala mbalimbali kupitia nfumo wa "majadiliano ya hoja" (debates). Hata hivyo, inaonekana kana kwamba hitimisho ya yale wanayoyajadili wadau yamekuwa yakiishia kwenye mitandano au makabati ya vyombo kama hivi.
Nadhani ipo haja kuangalia upya mfumo tunao kwenda nao, tumeona jinsi tunavyopoteza wasomi kupitia siasa, wengi wanataka kuwa waheshimiwa ili walipo wengine waendelee kuwaheshimu tu hata kama hawana mchango mkubwa kwa Taifa. Sasa Bunge la Jamhuri ya Muungano limejaa wadaktari na maprofesa. Bunge kama chombo cha Serikali ambacho kinaundwa na asilimia kubwa ya wajumbe wa chama Tawala, limepoteza kabisa mvuto na meno ya kuiuma Serikali ya chama chao kwa hofu iliyojengeka miongoni kwa waliomo kuwa ni usailiti kwa Chama, usaliti ambao unaweza kukupoteza kabisa katika ulingo wa siasa...
Hali inatisha...tunakoenda ni kiza kizito sana!!!
NAUNGA MKONO HOJA..