Ni hii mistari mitatu tu; actually miwili uliyoweza kuiwasilishai mada yako ili tuijadili kwa kina hapa JF?
Ninaelewa unayo mengi ya kujadili, lakini kama ilivyo kawaida yetu na elimu zetu hizi, inakuwia vigumu sana kuwasilisha andiko la mawazo hayo hapa ukumbini.
Pole yako na pole kwa nchi yetu hii Tanzania. Sote tumekuwa na upungufu mkubwa sana kutokana na kutekwa na CCM kwa kila njia na kutuweka katika kilema hiki.
Lakini nikubaliane nawe kwa hayo uliyoweza kuwasilisha hapo.
Inajulikana kwamba dola bilioni 17 na zaidi zimekwishatumiwa na taifa hilo kama msaada wa silaha kwa hao waliowaweka kama chambo chao tokea February, wakati walipovamiwa.
Sasa wewe fikiria, hiyo dola bilioni 17, ni pesa ndefu sana hasa kwa nchi zetu hizi. Hawa watu siku moja ingetokea kama muujiza hivi, wakaamua kutumia kiasi hicho cha kitita, kusaidia tu tuondokane na ukilema wetu huu wa kushindwa hata kuwasilisha tu mada, si hapo hali yetu ingebadilika sana?
Nimechangia kwenye mada yako hii, kwa sababu nimevutiwa na mwelekeo wa uamini wako, hata kama huwezi kuuwasilisha vyema tukakuelewa.