Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Kwa sababu sisi wanaume - ambao ndio tumeandika hizi sheria - tunataka kuendelea kuwatumia wanawake kama chombo cha ngono.
Kuhusu Sarah Palin, yule mkwe wake mtarajiwa hajaonekana ni mbakaji kwa kumtia mimba mtoto wa miaka 17 kwa vile na yeye pia ni mtoto. Sisi sheria yetu ya statutory rape ya mwaka 1998 mtoto wa kiume wa miaka 12 anaweza kubaka msichana mkubwa kuliko mvulana! Yani, konda wa miaka 15 akimjamia msichana wa miaka 17 atakuwa amembaka.
Yule msichana wa miaka 17 karubuniwa - na hivyo kisheria kabakwa - na mtoto mvulana wa miaka 15. Kwa maneno mengine wanawake akili zao hazikuwi haraka kuliko za watoto wa kiume. Ujuha mwingine huo!
Tubadilishe hii sheria ya 1998 ili watoto wakijamiana wenyewe kwa wenyewe kitoto cha kivulana cha miaka 14 kisiambiwe kimembaka msichana wa miaka 17 na nusu!
Tunashindwa mpaka kuandika sheria zenye mantiki, huwezi kuniambia UDSM ni moja ya vyuo vilivyo juu katika orodha ya vyuo bora Afrika.
Kuhani ukumbuke kuwa sheria ilikuwa lobbied na wana uamsho na TAMWA au to be specific wanawake waliokuwa frustuated kutokana na matatizo ya ndoa zangu kuwa makubwa na hatimaye kuvunjika. Mtu yoyote mwenye akili timamu hawezi kukubaliana na sheria hiyo kama unavyojua kuna baadhi ya mambo yanatokea Tanzania tu. Jaribu kuangalia Profile za wana Tamwa na hao wanauamsho utaona kimaadili ya kitanzania hawafit, hoa ndio walio lobby sheria hiyo ipitishwe lengo kubwa likiwa kupambana na wanaume na kuwakomoa, na cleary shera hiyo inamuona mwanaume kama dudu hivi na kibaya zaidi inamuona mwanamke kama kitu, ndio maana unaona mwanamke mwenye miaka 18 ni mtoto kuliko kivulana chenye miaka 14, sijui kama hilo hasa ndio lengo lao.
Cha ajabu sheria inasema mwanamke mwenye miaka chini ya 18 anabakwa, lakini nafahamu kuna vivulana vyenye miaka 16, 17 vikiwapa mimba wanawake wakubwa au hata wanawake walimu wao hawaoni kama hilo ni kosa, so pathetic.