This is pathetic

This is pathetic

Tatizo ni kuwa ukileta hii hoja jukwaani ( sizungumzii JF tu) kuna watu wataipinga kwa kigezo cha dini au tamaduni. Kuna watu walishafikia kuwa umri huu upunguzwe kufikia angalau miaka 14! Na wanaosema hivyo wana wajukuu wenye umri kama huu. Hawa wakuu wanapodai hivyo si kwa nia ya kuruhusu watoto waoane, la hasha! Hawa wanalenga vijibabu vyenzao. Sheria ibadilishwe ili mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka kumi na nane asiruhusiwe kujamiana na mtu mwenye umri wa chini ya umri huo!

Hiyo ya UDSM sina comment. Hao hao ndiyo watu waliopongezana kwa kushinda Nobel Prize mwaka jana!!!!
 
Kwa sababu sisi wanaume - ambao ndio tumeandika hizi sheria - tunataka kuendelea kuwatumia wanawake kama chombo cha ngono.

Kuhusu Sarah Palin, yule mkwe wake mtarajiwa hajaonekana ni mbakaji kwa kumtia mimba mtoto wa miaka 17 kwa vile na yeye pia ni mtoto. Sisi sheria yetu ya statutory rape ya mwaka 1998 mtoto wa kiume wa miaka 12 anaweza kubaka msichana mkubwa kuliko mvulana! Yani, konda wa miaka 15 akimjamia msichana wa miaka 17 atakuwa amembaka.

Yule msichana wa miaka 17 karubuniwa - na hivyo kisheria kabakwa - na mtoto mvulana wa miaka 15. Kwa maneno mengine wanawake akili zao hazikuwi haraka kuliko za watoto wa kiume. Ujuha mwingine huo!

Tubadilishe hii sheria ya 1998 ili watoto wakijamiana wenyewe kwa wenyewe kitoto cha kivulana cha miaka 14 kisiambiwe kimembaka msichana wa miaka 17 na nusu!

Tunashindwa mpaka kuandika sheria zenye mantiki, huwezi kuniambia UDSM ni moja ya vyuo vilivyo juu katika orodha ya vyuo bora Afrika.

Kuhani ukumbuke kuwa sheria ilikuwa lobbied na wana uamsho na TAMWA au to be specific wanawake waliokuwa frustuated kutokana na matatizo ya ndoa zao kuwa makubwa na hatimaye kuvunjika. Mtu yoyote mwenye akili timamu hawezi kukubaliana na sheria hiyo, kama unavyojua kuna baadhi ya mambo yanatokea Tanzania tu, hili ni moja wapo. Jaribu kuangalia Profile za wana Tamwa na hao wanauamsho, utaona kimaadili ya kitanzania hawafit au naweza kusema they are morally rotten, na hao ndio walio lobby sheria hiyo ipitishwe lengo kubwa likiwa ni kupambana na wanaume walioshindwa kuishi nao na kuwakomoa, na cleary shera hiyo inamuona mwanaume kama dudu hivi na kibaya zaidi inamuona mwanamke kama kitu, ndio maana unaona mwanamke mwenye miaka 18 ni mtoto kuliko kivulana chenye miaka 14, sijui kama hilo hasa ndio lengo lao.
Cha ajabu sheria inasema mwanamke mwenye miaka chini ya 18 anabakwa, lakini nafahamu kuna vivulana vyenye miaka 16, 17 vikiwapa mimba wanawake wakubwa au hata wanawake walimu wao hawaoni kama hilo ni kosa, so pathetic.
 
Kuhani ukumbuke kuwa sheria ilikuwa lobbied na wana uamsho na TAMWA au to be specific wanawake waliokuwa frustuated kutokana na matatizo ya ndoa zangu kuwa makubwa na hatimaye kuvunjika. Mtu yoyote mwenye akili timamu hawezi kukubaliana na sheria hiyo kama unavyojua kuna baadhi ya mambo yanatokea Tanzania tu. Jaribu kuangalia Profile za wana Tamwa na hao wanauamsho utaona kimaadili ya kitanzania hawafit, hoa ndio walio lobby sheria hiyo ipitishwe lengo kubwa likiwa kupambana na wanaume na kuwakomoa, na cleary shera hiyo inamuona mwanaume kama dudu hivi na kibaya zaidi inamuona mwanamke kama kitu, ndio maana unaona mwanamke mwenye miaka 18 ni mtoto kuliko kivulana chenye miaka 14, sijui kama hilo hasa ndio lengo lao.
Cha ajabu sheria inasema mwanamke mwenye miaka chini ya 18 anabakwa, lakini nafahamu kuna vivulana vyenye miaka 16, 17 vikiwapa mimba wanawake wakubwa au hata wanawake walimu wao hawaoni kama hilo ni kosa, so pathetic.

Kosa sio la wanawake wa TAMWA.

Huwezi hata siku moja kumlaumu lobbyist, isipokuwa aliyeandika sheria. Na, yeyote aliyeandika, hatimae ilipitishwa na Bunge. Lilaumu Bunge na Chenge. Kingine, ile sheria ya ndoa inayoruhusu kuolewa na miaka 15 iliandikwa mwaka 1971, na sidhani kuna mwanamke alishirikishwa pale. Ndio maana inasema mwanamme anaweza kujiolea idadi anayotaka. Ni wanaume tu wametawala kwenye hizi sheria baka-baka!

Na cha muhimu, sidhani kama ile sheria ya 1998 iliyoleta statutory rape ina lengo la kukomoa wanaume. Wasichana wadogo inabidi walindwe dhidi ya kina Maumba. Tatizo ni pale inapomchukulia mtoto wa kivulana mwenye umri mdogo kuliko msichana kama ni mbakaji. Na tatizo la hatari zaidi ni ile sheria ya ndoa ya 1971 inayosema mtoto wa miaka 15 anaweza kuolewa. Ni sheria ya wanaume inayofadhili ubakaji wa watoto kwa jina la ndoa.
 
Back
Top Bottom