kwa Mara nadhani ni wakurya, ambapo sio wote lakini, ni baadhi ya wazee tena wa kiume, ambao huwa wanaheshimika kama chief vile kwenye jamii yao, wao huitwa "wasubi" au "omusubhi" kwa kikurya, omusubhi akifariki huzikwa akiwa ameketi kwenye kiti CHAKE CHA ENZI pamoja na nyenzo zao zote walizokuwa wakizitumia kikazi wakati wa uhai wao. siku hizi wapo wachache sana na ni watu wa kuogopwa sana ndani ya jamii yao.
ukuryani ukikosea huyu msubi ndo huwa anatoa uamuzi wa mwisho ni adhabu gani upewe, yeye huwa kama jaji vile, anaweza kukupa adhabu ya kuhama kijiji au kulipa ngómbe kwa uliemkosea, au ukalipa kwa jumuia yote.
pia wanakuwa na madaraja kulingana na uwezo wao wa kufanya mambo, ambapo mara nyingi hii hutegemea na nguvu kali za giza walizo nazo, kwa mfano ukiweza mloga msubi, jaji alieko madarakani kwa muda huo, na akafa, wewe ndo unakuwa bingwa wa eneo hilo. huwa wana kawaida ya kutembea na usinga, (mkia wa ngómbe) hasa wanapokuwa kwenye sherehe kuonyesha kuwa yeye ndio big man wa eneo hilo.