Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Wazee wastaafu wa EAC wazuia magari ofisi za Hazina Dar
*Wapiga mawe gari la serikali mbele ya polisi
Na Fidelis Butahe
MIGOMO na harakati za kudai haki ambazo zimekuwa zikitapakaa kwa sura tofauti nchini, jana iligeukia kwa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati walipozuia magari kutoka na kuingia majengo ya Wizara ya Fedha na kulipasua kioo gari moja lililokaidi.
Wazee hao ambao wamekuwa wakidai malipo hayo kwa muda mrefu, jana walionekana kupandwa na hasira zaidi na kufanya kitendo hicho cha aina yake.
Baada ya kusababisha usumbufu kwa kuzuia magari kuingia au kutoka kwenye maeneo ya Wizara ya Fedha, Polisi waliitwa eneo hilo na kujaribu kuwatoa kwa nguvu, lakini ilishindikana.
Baadaye Polisi waliamua kumwambia dereva wa gari moja aina ya Land Rover Defender kuwa apitishe gari bila ya kujali kama kuna watu barabarani. Lakini wakati dereva huyo wa gari lenye namba za usajili, STJ 6157 akijiandaa kutekeleza amri hiyo, alistukia kioo cha mbele kikiwa kimepigwa mawe na kupasuka.
Baada ya tafrani hiyo dereva huyo alishuka kusubiri maelekezo zaidi, huku Polisi wakionekana kujirudi na kuacha kutumia nguvu.
Tukio hilo ni mwendelezo wa wimbi la matukio kadhaa ya kudai haki ambayo yamekuwa yakifanywa kwa njia ya migomo kote nchini, ikiwemo migomo iliyotikisa nchi kama ule wa wafanyakazi wa benki ya NMB na mgomo unaoendelea wa walimu.
"Tumechukua hatua hii kupinga kauli iliyotolewa juzi na Naibu Waziri wa Fedha, Omary Yusuph Mzee kuwa baadhi ya wastaafu ni vibarua na kwamba malipo yatakayofanyika ni kwa wale waliokuwa waajiriwa wa Jumuiya ya `Afrika Mashariki." alisema Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Nathaniel Mlaki.
"Sisi hatukuja hapa kwa shari, la hasha. Tulikuja hapa kutaka maelekezo kutoka kwa Waziri kwamba atatulipaje fedha tunazodai.
"Hizi fedha ni haki yetu kulipwa na tunachokitaka ni tume tuliyoiunda ihusishwe na wizara katika kuhakiki malipo yetu. Tukiwaacha wenyewe wanaweza kutulipa hata Sh 200 hawa".
"Na hili tulimwambia Naibu Waziri, lakini mpaka sasa hataki kuelewa maombi haya... eti serikali inasema tumeshalipwa, labda waeleze walitulipa wapi na lini."
Alisema kama kuna wastaafu ambao wameonekana kuwa hawastahili kulipwa basi ufanyike utaratibu wa kuwapa barua ambazo zitaeleza sababu za kutolipwa mafao yao, lakini si kama waziri alivyowatamkia kuwa vibarua hawatalipwa.
"Unajua nashindwa kumwelewa huyu waziri. Kwanza hapa hakuna kibarua. Vibarua wa enzi zile walikuwa wakifanya kazi miezi sita sita. Hawa wote unaowaona hapa wamefanya kazi zaidi ya mwaka mmoja na nusu... huoni hii kama ni dharau," alihoji Mlaki.
Jana wazee hao walikuwa wamekaa katikati ya barabara na kuendelea na mikakati ya jinsi ya kuendeleza harakati zao za kudai haki, ikiwa ni pamoja na kupeana karatasi ambazo zina vielelezo vinavyoeleza kiasi wanachostahili kulipwa.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wa vikundi vya wastaafu wa Jumuiya hiyo, Nathaniel Mlaki, wazee hao walitanda nje ya majengo ya Wizara ya Fedha na Uchumi, huku wengine wakiwa wamekaa katikati ya barabara na kusababisha magari yaliyokuwa yakitoka na kuingia wizarani humo kushindwa kupita.
Naibu Waziri Omary Yusuph Mzee alishatoa tamko kuwa majina ya watakaolipwa na wasiostahili kulipwa yataanza kubandikwa leo kwenye ukumbi wa Karimjee.
Afisa itifaki wa wizara hiyo, Cyprian Kuyava alisema wizara itaanza kubandika majina ya wanaostahili na wasiostahili kulipwa leo kwenye ukumbi wa Karimjee.
Akizungumzia kuhusu wazee wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, afisa huyo alisema kazi ya wizara si kukaa na wazee hao na kujadili kwa pamoja malipo yao bali ni kuwalipa pesa walizohakiki na kama kutakuwa na mapungufu katika ulipaji basi taratibu nyingine zitafuatwa.