Phil usiogope sana, kwa bahati nzuri miongoni mwa watu wenye uwezo huo wa kumpindua Kikwete hakuna mwenda wazimu, na kwanza ni watu wake damdam, kwa hiyo halitatokea hilo. Mkuu wa majeshi Gen Davis Adolf Mwamunyange ni mshikaji wake tangu wakiwa jeshi. IGP Saidi Ali Mwema ni shemeji yake. DG wa TISS Rashid Othman wametoka nae mbali, tangu kabla ya enzi zake pale MOFA ambako kamtunza sana. Kwa ujumla hakuna wa kumpindua JK, uwe na amani.
Hii ya kwake ni tofauti sana na Obote ambae aliweka mtu asiyetabirika, Idd Amin kuwa mkuu wa majeshi, amnaye hatimaye alimgeuka. JK ni mjanja zaidi, hana watu dizaini hiyo. Tatizo lililoko ni kuwa jinsi watu wanavyozidi kupungukiwa uvumilivu na kufanya fujo, ndivyo watawala wanavyozidi kupata visababu vya kutenda dhuluma kwa visingizio vya "law and order", na kama busara haitatumika hali itazidi kuwa mbaya siku baada ya siku.