This is too much.. Wazee nao warusha mawe Hazina!

This is too much.. Wazee nao warusha mawe Hazina!

Duh! yaani bado hawajawalipa tu mafao yao? What is the problem?

Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjika tangu 1977, waliokuwa wafanyakazi wa EAC toka Kenya na Uganda walishalipwa mafao yao miaka mingi tu. Hawa Wabongo wenzetu bado wanazungushwa tu kila kukicha miaka 31 tangu Jumuiya ivunjike!!! Tukiita serikali ya dhuluma na ya kifisadi wanakasirika.
 
.....nakumbuka kuna wakati wastaafu wa EAC walipewa cheque zao (correct me if im wrong).......sasa hawa wengine wametokea wapi?........au kuna wengine waliachwa!!.....kama waliachwa je ni kwa misingi gani?

Hivi serikalini hakuna mtu wa ku-clarify hili jambo now and then kila linapoibuka..........kama kuna mikataba waliyokuwanayo basi iwekwe wazi ili tujue maslahi yao yakoje.........sio kuwa mabubu mpaka watu wanarusha mawe..........

..............Trust me nyie waserikali kama mnafanya kazi zenu kisawasawa........hakuna atayewarushia mawe............
 
Tuna serikali ndugu yangu!!!!? Malalamiko yanaongezeka kila kona ya nchi kuhusu mafisadi, wanafunzi wa vyuo wanalalama kuhusu gharama za masomo na kutopatiwa mikopo wakati unaostahili, waliohamishwa makazi yao ili kuwapisha 'wawekezaji' wachimbe dhahabu hawajalipwa mafao yenye haki, mikataba isiyo na maslahi ya madini yetu, walimu na wafanyakazi wengine kudai haki zao kudai haki zao bila mafanikio yoyote na kutishia migomo, Kiwira kukwapuliwa na fisadi Mkapa, wazee wa EAC kupigwa chenga kuhusiana na haki zao yote haya serikali inajifanya kama haiyasikii na kuonyesha kama vile kila kitu kiko shwari. Waswahili walisema panapofuka moshi.....
 
.....nakumbuka kuna wakati wastaafu wa EAC walipewa cheque zao (correct me if im wrong).......sasa hawa wengine wametokea wapi?........au kuna wengine waliachwa!!.....kama waliachwa je ni kwa misingi gani?

Hivi serikalini hakuna mtu wa ku-clarify hili jambo now and then kila linapoibuka..........kama kuna mikataba waliyokuwanayo basi iwekwe wazi ili tujue maslahi yao yakoje.........sio kuwa mabubu mpaka watu wanarusha mawe..........

..............Trust me nyie waserikali kama mnafanya kazi zenu kisawasawa........hakuna atayewarushia mawe............

Mkuu Ogah,

Maneno mazito, unajua hata mzazi wangu anawadai kwa hela za bongo sasa, aliniambia ni karibu millioni 60 za mafao yake huko EAC kwa hiyo tuko wengi tunaozisubiria bro!
 
Hapa utaambiwa mchochezi

Hao kwa kupinduapindua maneno wanavyotaka wao si ndiyo wenyewe? Mimi nasema kweli kama wanaona kusema kweli ni uchochezi basi na iwe hivyo. Warioba naye atakuwa ni mchochezi na Watanzania wengi katika kona mbali mbali za nchi yetu walioamua kusema kweli kuhusu hali ya nchi yetu nao ni wachochezi. Wanaongezeka kila kukicha.
 
...uchaguzi ukifanyika kesho hao ndio wa kwanza kuipigia CCM kura na ndio hao hao waliotuwekea serikali ya CCM miaka yote hii,labda watajifunza!
 
.....nakumbuka kuna wakati wastaafu wa EAC walipewa cheque zao (correct me if im wrong).......sasa hawa wengine wametokea wapi?........au kuna wengine waliachwa!!.....kama waliachwa je ni kwa misingi gani?
Hivi serikalini hakuna mtu wa ku-clarify hili jambo now and then kila linapoibuka..........kama kuna mikataba waliyokuwanayo basi iwekwe wazi ili tujue maslahi yao yakoje.........sio kuwa mabubu mpaka watu wanarusha mawe..........
..............Trust me nyie waserikali kama mnafanya kazi zenu kisawasawa........hakuna atayewarushia mawe............

Ogah,

Kusema kweli si wewe peke yako unayetatizwa na jambo hili. Kosa kubwa la kwanza ni kujaribu kuwaweka hawa wastaafu kwenye kundi moja na wastaafu wa kawaida wa serikali wanaodai mafao yao. Ukweli ni kuwa fedha wanazodai ni zile zilizokabidhiwa kwa serikali kuwafikishia kwa vile tu waliotoa fedha hizo hawakuwa na njia ya kuwafikia. Serikali ndicho chombo kilichoaminiwa kuwa hakingewaibia wananchi wake na hivyo fedha hizo zingekuwa salama mpaka wenyewe (wastaafu) wazichukue.

Hizo fedha hazikutakiwa kuingizwa kwenye budget ya serikali bali kutunzwa benki kuu na wahusika wakishapatikana waandikiwe cheki kulingana na mahesabu yaliyoendana na mkataba wa EAC. Hiyo ilikuwa mwaka 1984 na makubaliaono yalikuwa walipwe kulingana na thamani halisi ya dola ya marekani. Kwa sababu zisizoeleweka serikali badala ya kuwalipa wahusika, iliamua kutumia fedha hizo kwa mazingira yasiyoeleweka kitendo ambacho kwa vyovyote ni wizi (serikali kuwaibia wananchi wake).

Inasemekana hizi fedha zilitumiwa siyo na serikali bali viongozi kwa kununulia mali huko ughaibuni kama nyumba za bei mbaya, magari ya fahari n.k. Mwishowe serikali ikajikuta haina tena fedha za kuwalipa wahusika na kuanza kufanya ujanja ujanja na wakati mwingine kutumia vitisho na dola kuwaziba mdomo wastaafu hao. MAFISADI wakati huo walifikiria hawa wastaafu watakaa kimya na baada ya muda wataanza kuitwa kwa Muumba moja baada ya mwingine na kweli wengi wamekufa bila kupata haki yao.

Mambo wanayofanyiwa hawa wazee, yangeweza tu kutendeka Tanzania tu eti nchi ya amani na upendo. Adhabu ya wahusika kwenye nchi zenye ustaarabu na sheria hao viongozi ni wa kufikishwa mahakamani na adhabu yao ni firing squad, period.
 
Phil usiogope sana, kwa bahati nzuri miongoni mwa watu wenye uwezo huo wa kumpindua Kikwete hakuna mwenda wazimu, na kwanza ni watu wake damdam, kwa hiyo halitatokea hilo. Mkuu wa majeshi Gen Davis Adolf Mwamunyange ni mshikaji wake tangu wakiwa jeshi. IGP Saidi Ali Mwema ni shemeji yake. DG wa TISS Rashid Othman wametoka nae mbali, tangu kabla ya enzi zake pale MOFA ambako kamtunza sana. Kwa ujumla hakuna wa kumpindua JK, uwe na amani.

Hii ya kwake ni tofauti sana na Obote ambae aliweka mtu asiyetabirika, Idd Amin kuwa mkuu wa majeshi, amnaye hatimaye alimgeuka. JK ni mjanja zaidi, hana watu dizaini hiyo. Tatizo lililoko ni kuwa jinsi watu wanavyozidi kupungukiwa uvumilivu na kufanya fujo, ndivyo watawala wanavyozidi kupata visababu vya kutenda dhuluma kwa visingizio vya "law and order", na kama busara haitatumika hali itazidi kuwa mbaya siku baada ya siku.

RAFIKI MKUBWA WA KIKWETE ALIKUWA LOWASA NA RAFIKI MKUBWA WA NYERERE ALIKUWA KAMBONA.so muda ukifika utasikia tu
 
Hili la hawa Wazee aliyezembea sio Kikwete ni Mwalimu. Limekaa muda mrefu, rekodi nyingi zimepotea, waliokwisha lipwa wanadai walipwe tena kutokana mkanganyiko huu wa kumbukumbu, wengine wala hawakuwahi kuwa waajiriwa wa EAC, watumishi wa hazina nao wanatumia vurugu hii kujineemesha,.....
 
Good point, WildCard. I hate this Kikwete guy, ila hapa nitamtetea. Huu ni uzembe wa Mchonga.
 
Natamani akae kimya hivyo hivyo na wala asishughilikie kitu ili yamkute,na kama utakua mwanzo wa ukombozi itakua heri.

Zaidi ya yote,aendelee kuwa bubu hadi hu mwaka uishe,chaguzi za mitaa zinakuja na hataweza kufanya kitu halafu 2010 iibuke.Wananchi watakua wamejaa hasira,kwa hiyo pia watapiga kura za hasira
 
Mkuu Ogah,

Maneno mazito, unajua hata mzazi wangu anawadai kwa hela za bongo sasa, aliniambia ni karibu millioni 60 za mafao yake huko EAC kwa hiyo tuko wengi tunaozisubiria bro!
na mie nasubiria tu za mzee wangu, kulipa washalipa ndiyo lakini hawakulipa inavyotakiwa ndio maana malalamiko yapo, wanadhania wanaweza dhulumu jasho la watu hivi hivi, mie mzee hadi anakaribia kufa aliniambia mahesabu ya haki zake zote yanakaribia m.100 kwa rate za wakati huo, na hiyo ilikuwa miaka 6 iliyopita.
 
Hii inanikumbusha mwanahalisi walichora katuni ya mama akimnyonyesha mwanae na kumwambia ajifunze kugoma kunyonya ili akiwa mkubwa asipate shida ya kudai haki zake ukubwani.
 
Tatizo Rais wetu ni mpole mno kwa wapambe wake. Bora basi angekuwa hata anatulia ofisini, lakini kila siku hayupo kwa hiyo watendaji wake nao wanajifanyia mambo yao watakavyo wao wenyewe!

Nahisi hata Lowasa anajilaumu kwanini alijiuzulu, maana naye angekomaa pengine angekuwa bado anaula tu madarakani!
 
is somebody losing control of this nation? Kwa sababu matokeo yake ni watawala kuanza a system of suppression.... inanikumbusha kisa cha Mugabe na Matebele....

Not only somebody's grip of this nation is loosing; no, it is that there is a remote control disrailing this nation out of its way.. au kwa ufupi ni kwamba raisi si huyo tumwonaye, kunmaraisi wengine wanatawala nchi hii kwa remote..
 
Back
Top Bottom