QM,
Ukiamini katika ukristo unatakiwa kutokuwa na shida na picha hiyo, maana iliandikwa bin-adam aende kukaa na kuijaza dunia na kuvitawala vyote vilivyomo, kutawala ni pamoja na kuchinja huko.
Tena ukifika sehemu sehemu huko kwenye mila za kunyumba watu wanatoa na sadaka ya damu bado.
Sasa tatizo ni hiyo idea ya kuchinja au kuiweka kwenye gazeti?
Kama hatuna tatizo na idea ya kuchinja, na tunapenda nyama, kwa nini kujifaragua kwamba picha hii haifai kuwekwa kwenye gazeti?
Akija rastafarian, au animal rightists tree hugger vegetarian akasema hivyo nitamuelewa kwa sababu ana principle za kutokula nyama na ukatili kwa wanyama, je wewe ni mmoja wao?
Mimi nafikiri, kama unataka ku protest, the issue should be mbuzi anachinjwa, na sio picha ya mbuzi anachinjwa iko front page.
Sisi na wamagharibi tuna value systems tofauti, muulize Rupia aliyekamatwa kwa kuchinja mbuzi nyumbani kwake.
There is a reason George Bush alisoma "My Pet Goat" and a pet is considered a member of family so in the US kumchinja mbuzi kunaweza kuwa interpreted sawa na kumchinja member of family.
Kama unakula nyama halafu hutaki ijulikane nyama inatoka wapi utakuwa unasimamia obscurity tu.