Wazee naona wanazidi kumuandama SIMBA LA KIKE!!!
Mwenyekiti wa Baraza la wazee wa Agikuyu Bw Wachira Kiago amemtaja Bi Millie Odhiambo kama mtoto mpotevu aliye na mkondo mrefu wa kimaisha kujinusuru kutokana na ukaidi na utundu wa bure na ambao haumwongezei heshima miongoni mwa wengi wanaoelewa wazi kuwa heshima si utumwa.
BARAZA la wazee wa Agikuyu Jumatano liliwataka wenzao kutoka Wajaluo limwandalie kikao cha dharura mbunge wa Mbita Bi Millie Odhiambo ili
kumkanya dhidi ya kutukana “wanaume wa jamii zingine.”
Kupitia mwenyekiti wake Bw Wachira Kiago, limesema kuwa “tumefedheheshwa sana na tabia ya mwanamke wa asili ya Luo kwa jina Bi Millie Odhiambo ambaye Jumanne alimtukana rais Uhuru Kenyatta kama mtoto wake mdogo.”
Bw Kiago akiongea Mjini Murang’a aliteta kuwa Rais Kenyatta kwanza ni mwanamume wa kijamii, mume na baba na ambaye kimila, hafai kutukanwa
hadharani na wanawake.
Bw Kiago alisema ni aibu kubwa kwa mwanamume yeyote kutukanwa hadharani huku ikiwa wazi kuwa bibi na watoto wake watapata ujumbe huo
wa matusi ukielekezwa kwa kiongozi wao wa familia.
“Hata ikiwa ungetaka kuonekana mtu shupavu ambaye hana uoga, tekeleza uhasama wako dhidi ya unayemchukia kwa njia za kistaarabu. Fanya
kampeni dhidi ya Rais ili asichaguliwe na wafuasi wako na katika ukumbi wa bunge, pinga mikakati yake kupitia mijadala iliyo na umakinifu wa busara ya maneno. Ufasaha wa lugha wa Bi Odhiambo ni aibu tele na ambayo inafaa kujadiliwa na wazee wa kwao,” akasema.
Hata hivyo, Bw Kiago alisema kuwa “ikiwa hakuna shida kwa wazee hao kumpata mwanamke wao akitukanana hadharani, basi waseme hivyo ili
wengine wanaodumisha nidhamu ya usemi katika hotuba kwa marika mbalimbali wakae wakijua Bi Odhiambo alikuwa na baraka za wazee wa
kwao."
Mila
Bw Kiago alisema ikiwa ni mwanamke wa Mlima Kenya ambaye alikuwa amenaswa akitoa matusi kama hayo ya Bi Odhiambo kwa mwanamume mwingine yeyote kutoka jamii yoyote ile, “kufikia sasa tungekuwa tumetoa masharti ya kutii na kumwadhibu kwa mujibu wa mila zetu.”
Alisema kuwa hata ikiwa wanawake wamejiangazia kama walio huru na walio na haki yao ya kumenyana kisiasa, “hakuna popote wameambiwa
kuwatusi wengine ni mojawapo ya haki hizo.”
Alimtaja Bi Odhiambo kama “mtoto mpotevu aliye na mkondo mrefu wa kimaisha kujinusuru kutokana na ukaidi na utundu wa bure na ambao haumwongezei heshima miongoni mwa wengi wanaoelewa heshima si utumwa.”