This man is either a sadist or alimuua kibaka, akanywa bia kusherehekea?



Acha kuzuga brother. Aliyemteua huyu mkuu wa mkoa wa Mbeya ndiyo yuleyule anayemuacha mkuu wa mkoa wa Dar kuendelea kupeta ilhali akiwa na tuhuma nyingi za ufisadi. Bandiko lako linakosa kuaminika unapokuwa unatoa matamko kama haya kwa baadhi ya viongozi wa serikali huku ukifumbia macho matendo ya viongozi wengine wa serikali.
 
Nchi za wenzetu huyu asingekua uraiani sasa hivi. Katoa ma ushahidi dhidi yake mwenyewe!

Kiukweli huyu si kiongozi ni mtawala anaona kuua ni sifa. Kuua ni sifa ya wanaotawala kiimla.

Kiongozi angetumia nafasi hiyo kujua nini kinafanya watu au vijana wawe vibaka. Tatizo ni nini na litatuliwe vipi na hiyo hadhira ingetoa mawazo na iwataje vibaka, akutane nao ajadiliane nao na kuwapa mawazo mbadala ili waache kuwa vibaka.

Kama hii nchi inatawaliwa na sheria, basi sheria ifuate mkondo wake.

Akijitetea alikua akichangamsha genge, basi avuliwe madaraka kwa sababu si mkweli, anatunga mambo na
kuyawasilisha mbele ya hadhara.
 
Ogopa katibu wako wa chama anongea kuhusu ukichaa wako hata masaa 24 hayajaisha unatoa kauli tata ujasiri unatoka wapi?

Huo sio ujasiri bali ni ujinga, mjinga ni yule anaefanya jambo bila kujua kama ni zuri au baya. Mjinga anafanya au kusema chochote, popote, muda wowote bila kufikiria au kujali athari ya matendo au maneno yake.
 
P, fanya mambo yako mengine achana na hayo. Utaulizwa maana ya Mayala law Kisukuma. Ccm wote wapo juu ya sheria, iko wazi. Kuna mtu alimpiga mtu risasi kanisani. Maisha yanaendelea.
 
Wewe mleta mada wewe! Kwahiyo umeshahitimisha kuwa ni kosa la hali ya akili ya mteuliwa na si kosa la aliyemteua. Unafikaje kwenye hitimisho hilo? Je, aliyemteua alitathmini hata kidogo tu kiwango cha uelewa cha aliyemteua? Au ndo ule uandishi wa style ya kung'ata na kupuliza ili angalau na wewe ukumbukwe kwenye teuzi?
 
Pascal, my friend, LIKE FATHER LIKE SON! Ile kauli ya "mnajua msaliti huwa anafanywa nini" ya baba yao ina madhara makubwa! Kupotea kwa akina Ben, Azory, sandarusi za maiti ufukweni bila kuchunguzwa na sababu za ajabu ajabu zlizotolewa na polisi wakati ule, they sent a go-ahead msg to those pretending to be "loyal" to the father! and hence such matamshi! Wanasema maovu na kutenda hawakemewi/kuadhibiwa, wonderful enough kinachofuata ni kupandishwa vyeo, what do you expect from others! UKWELI UNAUJUA WA CHANZO CHA MAOVU HAYA!
 
Ukiona umemuoa mwanamke mlevi kupindukia ujue wewe pia ni mlevi. Bila ChengA aliyemteua ndio chanzo cha vichaa kama hawa. Tuseme tu kazi ya punguani lazima upunguani udhirike kwa watu wote.


Na haya ndio matokea ya viongozi ambao hawatokani na sie wenyewe
 

Chini ya awamu hii, kiongozi kuwa katili ni sifa ya utendaji madhubuti. Na hii ni sifa toka viongozi wa juu kabisa kushuka chini. Fuatilia vizuri utabaini hilo.
 
Pascali wala usishangae na ukishangaaa zaidi utakuta kawa waziri ttzo lipo ktk ngazi ya uteuzi wew mpka katibu mkuuu kaongea mteuzi kimya muda haujaisha karudia kuharibu hawa si ndo wale hawafati sheria wanatuma watu kuandamana kudai ndege .shame on them hakuna wa afadhali na Paco unakujua sema unaogopa mataja anayewapa kiburi u najua vikao vya ndani huwa anawaaambia nn ? Simlaumu rc
 
ni aibu kwa mh. Rais kumuacha jamaa aendelee kuwa RC...kwa namna nyingine ni kama anaunga mkono maneno na matendo yake.
hata bashite ni walewale
Mkuu hii ni kauli ya Rais December 2018 "Polisi akiua muhalifu apandishwe cheo si kufukuzwa kazi, ilimradi haonei mtu "

Tofauti iko wapi hapo na hii ya huyu Chizi wa Mbeya?
 

Kuna wakati pia mwenyekiti aliwaambia policcm wawalaze chini watu fulani kama sijakosea..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…