Thomas Isidore Sankara: Taa ya AFRIKA iliyozimika ghafla ikiwa na umri mdogo wa miaka 38 kwa mapinduzi na kuuawa na Rafiki yake Kipenzi

Paploman

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2019
Posts
1,759
Reaction score
3,452
“While Revolutionaries as individuals can be murdered, you cannot kill Ideas”, Haya yalikuwa ni maneno ya Thomas Sankara aliyoyatamka wiki moja kabla ya kuuawa.

Thomas Sankara alikuwa kiongozi na akiwa na miaka 33 tu, Lakini mwenye maono makubwa na siasa za mrengo wa kushoto, anatambulika sana kama "Che of Africa"-‘Che wa Afrika’ akifananishwa na Ernesto Guevara ambaye alikuwa mwanamapinduzi huko Amerika Kusini. Thomas Isidore Noel Sankara alizaliwa Desemba 21 mwaka 1949 nchini Burkina Faso iliyotambulika Kama Upper Volta kwa wakati huo.”

Wakati wa mafunzo ya kijeshi alikutana na kapteni Blaise Compaoré wakawa marafiki wakubwa. Thomas Sankara alipanda ngazi za kijeshi hadi cheo cha Captain pamoja na rafiki yake Blaise Compaore

Mwaka 1981 alikuwa waziri wa mambo ya ndani katika serikali ya kijeshi ya Rais Jean Baptiste Major. Dr. na baadaye aliteuliwa kuwa waziri mkuu kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Januari 1983 mpaka mwezi Mei alipokamatwa na kutiwa mbaroni na serikali ya Rais Major Jean Baptiste Dr kutokana na msimamo wake juu ya ukombozi kwa watu wote wa Volta na kupendelea Marxist Revolution theories.

Mnamo august 1983, vijana wawili marafiki haswa pia makapteni wa jeshi na wanamapinduzi, Thomas sankara na blasius compaore walipindua serikali ya rais wa wakati huo katika nchi iliyojulikana kama upper volta, ya rais Baptiste Ouedraogo na Sankara kuwa Rais wa TANO wa VOLTA YA JUU au BURKINA FASO kwa sasa

Vijana hawa wakiwa katika fikra za kimax wakiwa na ndoto nyingi za kuijenga upper volta, walibadili kabisa historia ya taifa hilo, walibadili jina la nchi na kuitwa Burkina faso, maana yake nchi ya watu (country of honorable citizen), Sankara akawa anatumia baiskeli kutembelea vijijini kuhimiza maendeleo wakiwa na pacha wake compaore wakiwa kama pete na kidole.

Urafiki wa makapteni hawa ulikuwa mkubwa kiasi ambacho wakati wanausalama walipomwambia sankara kuwa compaore ana mpango wa kumpindua na kumuua yeye aliwajibu kuwa compaore asingeweza kufanya hivyo, Labda mtu mwingine. Akaongeza kuwa hata kama compaore angetaka kufanya hayo, hakuna wa kumzuia. Ni wazi kuwa sankara alikuwa karibu mno na compaore,kwa kiasi kuwa compaore alikuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya sankara

kama ilivyoambiwa na wanau usalama, compaore aliongoza mapinduzi yaliyosababisha kifo cha rafiki yake sankara mwaka 1987 October 5, na yeye mwenyewe huku akishuhudia rafiki yake kipenzi sankara akiuuwa katika mapigano ya usaliti yaliyotokea Mjini Ouagadougou Sankara akiwa katika kikao cha utendaji wa kazi, Akawa ndo rais mpya wa sita wa Bukinafaso.

Compaore, Alipata kusema katika shirika la kutetea haki za Binadamu duniani kwamba “kifo cha Thomasi Sankara ni ajali tu kama ajali zingine.

Cc
Proved , zitto junior , mtu chake

N:B

Habari hii ni kwa msaada wa machapisho, vitabu na site mbalimbali mtandaoni, binafsi nimejaribu kutafsiri tu kwa lugha ya Kiswahili kama kuna makosa tusahihishane.
 
Imepita miaka 33 tangu aliyekuwa Rais wa Burkina Fasso, Thomas Sankara(African Che Guavara) auawe na mabeberu(imperialists) wa Kifaransa.

Huyu mwamba aliwafukuza hawa mabeberu toka nchini mwake, kisha akaitoa nchi yake kwenye ushirikiano na IMF na kuifanya Burkina Faso isiwe tegemezi na misaada ya nje kabisa.

Mafanikio Yake Katika Kipindi cha Miaka 4 ya Uongozi Wake:
 
Attachments

  • IMG_20201028_113942.jpg
    IMG_20201028_113942.jpg
    180.1 KB · Views: 15
  • IMG_20201028_114447.jpg
    IMG_20201028_114447.jpg
    82.7 KB · Views: 16
  • IMG_20201028_114449.jpg
    IMG_20201028_114449.jpg
    75.1 KB · Views: 15
“While Revolutionaries as individuals can be murdered, you cannot kill Ideas”, Haya yalikuwa ni maneno ya Thomas Sankara aliyoyatamka wiki moja kabla ya kuuawa.

Thomas Sankara alikuwa kiongozi na akiwa na miaka 33 tu, Lakini mwenye maono makubwa na siasa za mrengo wa kushoto, anatambulika sana kama "Che of Africa"-‘Che wa Afrika’ akifananishwa na Ernesto Guevara ambaye alikuwa mwanamapinduzi huko Amerika Kusini. Thomas Isidore Noel Sankara alizaliwa Desemba 21 mwaka 1949 nchini Burkina Faso iliyotambulika Kama Upper Volta kwa wakati huo.”

Wakati wa mafunzo ya kijeshi alikutana na kapteni Blaise Compaoré wakawa marafiki wakubwa. Thomas Sankara alipanda ngazi za kijeshi hadi cheo cha Captain pamoja na rafiki yake Blaise Compaore

Mwaka 1981 alikuwa waziri wa mambo ya ndani katika serikali ya kijeshi ya Rais Jean Baptiste Major. Dr. na baadaye aliteuliwa kuwa waziri mkuu kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Januari 1983 mpaka mwezi Mei alipokamatwa na kutiwa mbaroni na serikali ya Rais Major Jean Baptiste Dr kutokana na msimamo wake juu ya ukombozi kwa watu wote wa Volta na kupendelea Marxist Revolution theories.

Mnamo august 1983, vijana wawili marafiki haswa pia makapteni wa jeshi na wanamapinduzi, Thomas sankara na blasius compaore walipindua serikali ya rais wa wakati huo katika nchi iliyojulikana kama upper volta, ya rais Baptiste Ouedraogo na Sankara kuwa Rais wa TANO wa VOLTA YA JUU au BURKINA FASO kwa sasa

Vijana hawa wakiwa katika fikra za kimax wakiwa na ndoto nyingi za kuijenga upper volta, walibadili kabisa historia ya taifa hilo, walibadili jina la nchi na kuitwa Burkina faso, maana yake nchi ya watu (country of honorable citizen), Sankara akawa anatumia baiskeli kutembelea vijijini kuhimiza maendeleo wakiwa na pacha wake compaore wakiwa kama pete na kidole.

Urafiki wa makapteni hawa ulikuwa mkubwa kiasi ambacho wakati wanausalama walipomwambia sankara kuwa compaore ana mpango wa kumpindua na kumuua yeye aliwajibu kuwa compaore asingeweza kufanya hivyo, Labda mtu mwingine. Akaongeza kuwa hata kama compaore angetaka kufanya hayo, hakuna wa kumzuia. Ni wazi kuwa sankara alikuwa karibu mno na compaore,kwa kiasi kuwa compaore alikuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya sankara

kama ilivyoambiwa na wanau usalama, compaore aliongoza mapinduzi yaliyosababisha kifo cha rafiki yake sankara mwaka 1987 October 5, na yeye mwenyewe huku akishuhudia rafiki yake kipenzi sankara akiuuwa katika mapigano ya usaliti yaliyotokea Mjini Ouagadougou Sankara akiwa katika kikao cha utendaji wa kazi, Akawa ndo rais mpya wa sita wa Bukinafaso.

Compaore, Alipata kusema katika shirika la kutetea haki za Binadamu duniani kwamba “kifo cha Thomasi Sankara ni ajali tu kama ajali zingine.

Cc
Proved , zitto junior , mtu chake

N:B

Habari hii ni kwa msaada wa machapisho, vitabu na site mbalimbali mtandaoni, binafsi nimejaribu kutafsiri tu kwa lugha ya Kiswahili kama kuna makosa tusahihishane.
 
Sankara alimkejeli Rais wa Ivory Coast Houphet Boigny na kumuita kibaraka wa mabeberu hususan Ufaransa. Campaore amemuoa mtoto wa Boigny. Boigny alikuwa na ushawishi mkubwa wakati huo, kikanda na kimataifa na aliheshimika kwa kuwa mtu senior wakati ule. Hakuna kiongozi ambaye alithubutu kumkejeli wazwazi isipokuwa Thomas Sankara. Now you can connect the dots by more readings.
 
Back
Top Bottom