Thomas Sankara (1949-1987) - Muasisi wa taifa la Burkina Faso

Thomas Sankara (1949-1987) - Muasisi wa taifa la Burkina Faso

Tujikumbushe kidogo kuhusu Kapteni Thomas Sankara, Rais wa zamani wa Burkinafaso 1983-1987. Rais kijana kabisa aliyechukua nchi katika umri wa miaka 33 tu katika mapinduzi ya mwaka ule wa 1983 katika nchi ile ya koloni la zamani la Wafaransa, zamani ikijulikana kama Volta ya Juu! Upper Volta. Sankara alikuwa na baiskeli moja na gari moja tu. Alipinduliwa na kuuawa jioni ya tarehe 15/10/1987. Aliyempindua alikuwa ni rafiki yake wa karibu sana. Kapteni Blaise Compaore. (your worst enemy could be your best friend, and your best friend your worst enemy) alipata kuimba Mwanamuziki Robert Nesta Marley. Mara kadhaa watu wa usalama walimtahadharisha Sankara kuwa rafiki yake huyo anapanga mipango na kula njama za kutaka kumuua. Yeye alikuwa anawajibu kuwa kama Compaore anataka kuniua basi hawezi kushindwa kitu maana anajua kila kitu kunihusu mimi!
I can imagine....when he was informed about the plot, a week before he was murdered he recorded his view so sadly...and said let him do it....it will be his problem...to betray a friend
 
Hii ya Compaore na Sankara imenisikitisha sana...urafiki ni kitu cha ajabu sana...

Mi naona ukichukulia kila urafiki ni business setting and nothing more ni bora kabisa...

Halafu majitu manafiki yakiona huyaamini yanaanza kulalamika "ooh huniamini",sijui nini...ni hatari sana.

Halafu naona Compaore mpaka leo anatawala tu nadhani...how can he last this long?

Sankara was trully a leader...check him up on youtube,really visionary leader!
 
Sankara alivyokufa ilinisikitisha sana!

Yaani unauliwa na childhood intimacy, class mate, room mate, baadaye mnakuwa co-worker!

Sema Compaore ana moyo hadi sasa, yaani lijamaa hata halistuki kuwa limecoup nchi due to kill one of his bestfriend!

Ila Compare mchongo wa kumuua Sankara alipanga na watu wazito, mpaka na baba mkwe sijui ni wa ivory coast ( alikuwa rais) ....kibaya zaidi ni jinsi wakina Compaore walivyomkaanga Sankara kwenye petrol, yaani hadi mfupa haukuonekana!

Ila iko siku Mwenyezi Mungu atamchapa Kofi na ufirauni wake! Hii Dunia hii...
 
Sitaki urafiki wa kidunia

Unafiki sana na kupotezeana dira za kimaisha!

Kiufupi ukimtoa mama angu mzazi, sitaki kiumbe chochote hapa chini ya jua kinijue, kinizoee!
Maneno huwa yanaumba siku mama yako mzazi hayupo ni nani atakuwa na wewe ?
Basi nakushauri fuga hata Mbwa atakufariji wakati wa kukupa faraja hayupo
 
Niliangalia documentary yake ambayo ilichukuliwa 1 month before afe... He's truly mwanamapinduzi! Huo mpango wa kumuua haukupangwa na huyo best friend wake tu serikali ya ufaransa nayo ilihusika kwa kiasi kikubwa
 
Huwa namuita the upright man...he was one of the African leader aliyekuwa anajielewa
 
thomas-sankara-1024x614.jpeg

Facts about Thomas Sankara in Burkina Faso

PREV ARTICLE NEXT ARTICLE


After renaming his country to Burkina Faso, here’s Thomas Sankara’s accomplishments, ONLY 4 YEARS in power (1983-87).

Thomas Isidore Noël Sankara (21 December 1949 – 15 October 1987) was a Burkinabé military captain, Marxist revolutionary, pan-Africanist theorist, and President of Burkina Faso from 1983 to 1987. Viewed by supporters as a charismatic and iconic figure of revolution, he is commonly referred to as “Africa’s Che Guevara”
  • Took power at 33 died at 37.
  • Make sure in four year the country is self sufficient in Food, cloth and everything else in four years no apologies, no excuses just did his job.
  • Killed by his best friend from childhood Blaise Compaore with help of France.
  • He initiated a nation-wide literacy campaign, increasing the literacy rate from 13% in 1983 to 73% in 1987.
  • All people who didn't have job he ask to help with building road, teaching, help in any way they can their community and ll get paid what government can afford instead of staying idle at home. And most people love the idea.
  • He planted over 10 million trees to prevent desertification.
  • He built roads and a railway to tie the nation together, without foreign aid. He never beg anybody including IMF or World Bank, France, UK or USA. Of course he was betrayed by his friend (brother).
  • He appointed females to high governmental positions, encouraged them to work, recruited them into the military, and granted pregnancy leave during education.
  • He outlawed female genital mutilation, forced marriages and polygamy in support of Women’s rights
  • He sold off the government fleet of Mercedes cars and made the Renault 5 (the cheapest car sold in Burkina Faso at that time) the official service car of the ministers.
  • He reduced the salaries of all public servants, including his own, and forbade the use of government chauffeurs and 1st class airline tickets.
  • He redistributed land from the feudal landlords and gave it directly to the peasants(poor without anything).
  • Wheat production rose in three years from 1700 kg per hectare to 3800 kg per hectare, making the country food self-sufficient.
  • He opposed foreign aid, saying that “he who feeds you, controls you.”
  • He spoke in forums like the Organization of African Unity against continued neo-colonialist penetration of Africa through Western trade and finance.
  • He called for a united front of African nations to repudiate their foreign debt. He argued that the poor and exploited did not have an obligation to repay money to the rich and exploiting
  • In Ouagadougou, Sankara converted the army’s provisioning store into a state-owned supermarket open to everyone (the first supermarket in the country).
  • He refused to use the air conditioning in his office on the grounds that such luxury was not available to anyone but a handful of Burkinabes.
  • As President, he lowered his salary to $450 a month and limited his possessions to a car, four bikes, three guitars, a fridge and a broken freezer.
  • A motorcyclist himself, he formed an all-women motorcycle personal guard. ( Adopted by Muammar Gaddafi Later)
  • He required public servants to wear a traditional tunic, woven from Burkinabe cotton and sewn by Burkinabe craftsmen. (The reason being to rely upon local industry and identity rather than foreign industry and identity)
  • When asked why he didn’t want his portrait hung in public places, as was the norm for other African leaders, Sankara replied “There are seven million Thomas Sankaras.”
  • An accomplished guitarist, he wrote the new national anthem himself
  • He vaccinated 2.5 million children against meningitis, yellow fever and measles in a matter of weeks.

  • His revolutionary programs for African self-reliance made him an icon to many of Africa’s poor. Sankara remained popular with most of his country’s impoverished citizens. However his policies alienated and antagonised the vested interests of an array of groups, which included the small but powerful Burkinabé middle class, the tribal leaders whom he stripped of the long-held traditional right to forced labour and tribute payments, and France and its ally the Ivory Coast. As a result, he was overthrown and assassinated in a coup d’état led by Blaise Compaoré on October 15, 1987 with help of France. A week before his murder, he declared: “While revolutionaries as individuals can be murdered, you cannot kill ideas.”

On October 15, 1987, Sankara was killed by an armed group with twelve other officials in a coup d’état organised by his former colleague Blaise Compaoré. Deterioration in relations with neighbouring countries was one of the reasons given, with Compaoré stating that Sankara jeopardised foreign relations with former colonial power France and neighbouring Ivory Coast.

Sankara’s body was dismembered and he was quickly buried in an unmarked grave, while his widow Mariam and two children fled the nation. Compaoré immediately reversed the nationalizations, overturned nearly all of Sankara’s policies, rejoined the International Monetary Fund and World Bank to bring in “desperately needed” funds to restore the “shattered” economy,[34] and ultimately spurned most of Sankara’s legacy. Compaoré’s dictatorship remained in power for 27 years until overthrown by popular protests in 2014.

A transformational leader
Sankara’s visionary leadership turned his country from a sleepy West African nation with the colonial designation of Upper Volta to a dynamo of progress under the proud name of Burkina Faso (“Land of the Honorable People”). He led one of the most ambitious programs of sweeping reforms ever seen in Africa. It sought to fundamentally reverse the structural social inequities inherited from the French colonial order.

Sankara focused the state’s limited resources on the marginalized majority in the countryside. When most African countries depended on imported food and external assistance for development, Sankara championed local production and the consumption of locally-made goods. He firmly believed that it was possible for the Burkinabè, with hard work and collective social mobilization, to solve their problems: chiefly scarce food and drinking water and they did.

In Sankara’s Burkina, no one was above farm work, or graveling roads–not even the president, government ministers or army officers. Intellectual and civic education were systematically integrated with military training and soldiers were required to work in local community development projects.

Sankara disdained formal pomp and banned any cult of his personality. He could be seen casually walking the streets, jogging or conspicuously slipping into the crowd at a public event. He was a rousing orator who spoke with uncommon candor and clarity and did not hesitate to publicly admit mistakes, chastise comrades or express moral objections to heads of powerful nations, even if it imperiled him. For example, he famously criticized French president François Mitterrand during a state dinner for hosting the leader of Apartheid South Africa.

Here at UN


Facts about Thomas Sankara in Burkina Faso | Africa Facts
 
[2:17AM, 7/11/2017]

: HUYU NDO THOMAS SANKARA RAIS MASKINI KULIKO WOTE KUWAHI KUTOKEA BARANI AFRIKA, MWENYE UZALENDO WA KUSHANGAZA.

Mnamo august 1983, vijana wawili, makapteni wa jeshi na wanamapinduzi, Thomas Sankara na Blasius Compaore, waliipindua serikali ya Rais wa wakati huo katika nchi iliyokuwa ikijulikana kama Upper volta, rais huyu aliitwa Baptiste Ouedraogo.

Vijana hawa wakiwa katika fikra za Karl Max, wakiwa na ndoto nyingi za kuijenga Upper volta, walibadili kabisa historia ya taifa hilo, walibadili jina la nchi na kuitwa Burkina faso, maanake nchi ya watu, country of honorable citizen.

Uchapakazi wa vijana hawa (Sankara na Compaore), Thomas sankara akiwa ndiye rais unaweza kufananishwa na ule wa Fider Castrol na Che Guavera, kabla haujachuja kule Cuba..

Haiyumkini Sankara alikuwa anatumia baiskeli kutembelea vijijini kuhimiza maendeleo, wakati pacha wake (Compaore) wakiwa kama pete na kidole.

Urafiki wa makapteni hawa wa jeshi la Burkinabe, ulikuwa mkubwa kiasi ambacho, wakati wanausalama walipomwambia Sankara kuwa Compaore ana mpango wa kumpindua na kumuua, yeye aliwajibu kuwa compaore asingeweza kufanya hivyo, labda mtu mwingine.

Blaise Compaore alikutana na Thomas Sankara mwaka 1976 katika mafunzo ya kijeshi Morocco na hapo walianza urafiki wao uliokuwa wazi kwa karibu watu wote waliokuwa wakiwafahamu nchini Burkina Fasso na nchi jirani.

Thomas Sankara alikuwa akiwaeleza wanausalama wake kuwa, hata kama Compaore angetaka kufanya hayo, hakuna wa kumzuia.

Ni wazi kuwa Kapteni Thomas Isidore Sankara alikuwa karibu sana na Blaise Compaore, kwa kiasi ambacho Blaise Compaore alikuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya Sankara.

kama ilivyotabiriwa na watu wengi wa karibu wa Thomas Sankara, Blaise Compaore aliongoza mapinduzi yaliyosababisha kifo cha Sankara mnamo mwaka 1987, na yeye mwenyewe (Compaore), huku akishuhudia rafiki yake kipenzi Sankara akiuwa, Akawa ndiye mrithi wa kiti cha Urais wa iliyokuwa Upper Volta baadaye Burkina Fasso.

Thomas Isidore Noël Sankara ni nani??

Isidore Noël Thomas Sankara alizaliwa tarehe 12.12.1949 Mjini YOKO katika nchi iliyokuwa ikiitwa Upper Volta (Volta ya juu) na kuuawa tarehe 15.10.1987 na wanajeshi wenzake wakiongozwa na rafiki yake Rais Blaise Compaore katika mapigano ya usaliti yaliyotokea Mjini Ouagadougou akiwa katika kikao cha utendaji wa kazi.

Thomas Sankara alipanda ngazi za kijeshi hadi cheo cha kaptenu pamoja na mwanajeshi Rafiki yake Blaise Compaore ANAYEJUA SIRI YA KIFO CHA CHA THOMAS SANKARA .

Kuna nyakati ambazo Blaise Compaore alipata kunena kwa kinywa chake katika shirika la kutetea haki za Binadamu duniani kwamba “kifo cha Thomasi Sankara kilikuwa ni ajali tu.

Mwaka 1981 Thomas Sankara alikuwa waziri wa mambo ya ndani katika serikali ya kijeshi ya Rais wa wakati huo wa Burkinabe ya zanani (Upper Volta) Jean Baptiste Major. Dr. na baadaye aliteuliwa kuwa waziri mkuu kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Januari 1983 mpaka mwezi Mei alipokamatwa na kutiwa mbaroni na serikali ya Rais Major Jean Baptiste Dr kutokana na msimamo wake juu ya ukombozi kwa watu wote wa Volta ya Juu na kupendelea Marxist Revolution theories.

Thomas Isidore Noël Sankara alikuwa Rais wa Upper Volta (Volta ya Juu) kuanzia mwezi Agosti 4 1983 hadi mwezi Octoba 15 1987 baada ya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Major Dr Jean Baptiste yakiongozwa na Blaise Compaore na kuwa Rais wa TANO wa VOLTA YA JUU au BURKINA FASO baada ya kubadilishwa jina na Sankara.

Thomas Sankara aliyejulikana kama Che – Guevara wa Afrika alianzisha Program mbalimbali za kijamii na kiuchumi kuleta mabadiliko katika nchi za Afrika. Alibadilisha Upper Volta na kuwa Burkina Faso (land of Upright Men).

Alianzisha kampeni ya kuboresha Elimu na kutanua
Huduma za Afya kwa watu wa Burkina Faso maeneo ya vijijini hasa kwa watoto walio athirika na magonjwa ya Uti wa mgongo , Homa ya manjano, na surua.. na watoto karibu milioni 3 walipata tiba hizo..

Pia alianzisha kampeni ya upandaji wa miti kitaifa, na takribani miti Milioni kumi ilipandwa nchi nzima..

Pia alianzisha kampeni ya usafi nchini kote, kila mwananchi alipaswa kufanya usafi eneo alipo na Sankara mwenyewe alikuwa anashika fagio na kuingia barabarani kufanya usafi. Hiyo ni kampeni iliyoitwa mfagio wa mwananchi (le balai citoyen).

Aliongeza idadi ya wanawake katika serikali yake, ikiwa ni kampeni yake nchi nzima kupinga tohara kwa wanawake, pia alianzisha kampeni na baadae utaratibu wa kisheria wa kuwataka wasichana waliopata mimba wakiwa mashuleni kuendelea na masomo pia akaajiri wanawake jeshini, akawapa ajira katika sekta za umma ili kupunguza unyanyasaji wa kijinsia na kuleta uwiano na usawa nchini Burkina Fasso.

Pia ndoa za wasichana wadogo na za kulazimishwa haswa za kimila katika maeneo mengi ya Burkina Fasso zikapigwa marufuku.

Thomas Sankara ambaye hakutaka makuu kabisa na wananchi wa Burkina Fasso. Akiwa kama Rais wa nchi, alivaa nguo zilizotengenezwa Burkina Faso badala ya suti kutoka Paris na London. mara nyingi alionekana akiwa kwenye gwanda la jeshi.

Pia Thomas Sankara alifuta matumizi ya magari ya kifahari kwa viongozi na watumishi wote wa umma, yeye kama Rais alikuwa akitumia baiskeli au miguu kwenda kwa wananchi vijijini kuhimiza na kusimamia shughuli za kimaendeleo.

Alijikita sana kwenye kusimamia na kukuza sekta ya afya katika Burkinabe, alihimiza watu kujihusisha na kilimo akiwapelekea zana za kilimo na pembejeo bure kwa watu wa vijijini na kugawa ardhi kwa wananchi ili wajihusishe na kilimo.

Kwa muda mfupi sana akiwa kama Rais wa Burikna Fasso, aliweza kuifanya nchi hiyo kuagiza chakula kutoka nchi za nje na kuifanya nchi hiyo kuanza kuuza vyakula vyake nje akaanza kuifanya Burkina Fasso kuwa imara kiuchumi.

Sankara aliwahimiza watawala wa Afrika waache kuwaibia wananchi, waache kutegemea sadaka kutoka nje.

Sankara akawaambia madeni ya Afrika hayana uhalali kwa vile yalitokana na mikataba mibovu.

Ndio maana hakuna maendeleo yaliyotokana na mikopo ya kigeni.

Sankara akataka Afrika iache kulipa madeni yasiyolipika.

Mwalimu Nyerere naye wakati huo alisema mtu hawezi kulipa madeni wakati watoto wanakufa njaa.

Thomas Sankara alisema ukitaka kujua maana ya ubeberu angalia sahani yako ya chakula, utaona kila aina ya chakula unachokula kinatoka nje. Ndipo akahimiza Afrika ijitegemee kwa chakula, akisema: "Anayekulisha anakutawala"

Thomas Isidoré Nöel Sankara ni wazi aliwakasirisha sana mabeberu wa kimagharibi, hasa ubeberu wa Kifaransa uliokuwa ukitawala kupitia vibaraka wake wa Afrika kama Rais Felix Houphouet- Boigny wa Ivory Coast.

Chini ya uongozi wake (Thomas Sankara), Burkina Faso ililima chakula chake badala ya kuagiza kutoka nje.

Kwa hatua hiyo, Thomas Sankara akawa amewaudhi wakubwa wa dunia (mabeberu) kwa kukataa kwake mipango ya kurekebisha uchumi ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) huku hoja kubwa ya sankara ikiwa ni kwamba, mipango hiyo ni ya kinyonyaji.

Thomas Sankara aligawa ardhi kwa wakulima wadogo baada ya kuchukua kutoka kwa wawekezaji wa nje ambao walikuwa wameipora baada ya kupewa na uongozi uliopita.

Katika huduma za jamii alileta mabadiliko makubwa katika huduma za elimu, afya, maji na kuboresha miundombinu ya barabara kuunganisha sehemu mbalimbali za nchi hiyo.

Sankara katika kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinahudumia wanachi wa kawaida, Sankara alipambana na rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma, huku akimtaka kila mwananchi kujituma kulijenga taifa.

Thomas Sankara alikuwa mtu anayechukia rushwa na ufisadi, uvivu, uzembe, dhuluma na unyonyaji wa wananchi na rasilimali zao. Alitaka kuona watu wake wakifaidika kwa rasilimali za nchi yake.

Huyu ndiye Thomas Sankara ambaye alipunguza mshahara wake hadi dola 450 kwa mwezi, ambaye alitembea kwa baskeli katika mitaa ya Ouagadougu bila ya kulindwa. Alipoulizwa kwanini hana walinzi alisema wananchi ndio walinzi wake, hivyo hahitaji kuambatana na wanajeshi wenye bunduki.

Washauri wake mara kwa mara walimshawishi aachane na matumizi ya baisikeli.

Akaamua kutumia gari lenye bei ya chini (Renault 5) badala ya msururu wa mashangingi kama tuonavyo leo katika Afrika...

Hata hivyo alibaki na baiskeli yake mpaka alipokutwa na mauti, na akaunti yake ya benki ilikutwa na akiba ya dola 400 ambayo ni sawa na Tsh 850, 550/= (laki nane elfu hamsini na tano namia tano hamsini), kwa sasa, badala ya mabilioni mengi kama wanayoficha huko Uswisi watawala wetu leo.

Kumbuka, Thomas Sankara amedumu kwenye uongozi kwa kipindi cha miaka 4 pekee kabla ya mapinduzi yaliyoongozwa na Rafiki yake kipenzi. Blaise Compaore ambaye aliondoka na uhai wake, lakini kwa kipindi hiko cha miaka 4 akihudumu kama Rais, alitengeneza mageuzi makubwa sana.

Ndoto kubwa ya kila siku ya Thomas Sankara, ilikuwa ni kuifanya Burkinafasso kuwa moja kati ya mataifa makubwa Afrika kiuchumi.

Thomas Sankara alikataa hata picha yake (yeye kama Rais) kutundikwa katika majengo, na taasisi za serikali alisema hataki kutukuzwa.

Sankara alikuwa akipokea mshahara wa dola 450 kwa mwezi, mshahara mdogo kuliko viongozi wote barani Afrika kwa wakati huo.

Huyu ndiye Thomas Isidore Noël Sankara anayejulikana kama Ernesto Che Guevara wa bara la Afrika (alikuwa akivaa mavazi kama Che Guevara, mwenendo, matendo na malengo yake yalifanana na Ernesto Che Guevara, pia walikuwa marafiki wakubwa), aliyeiongoza nchi kwa muda wa miaka minne kabla ya kuuliwa na maadui wa mapinduzi wakiongozwa na kapteni Blaise Compaoré Aliuliwa nyakati za usiku na mara moja akazikwa kwa haraka. Ernesto Che Guevara naye alikuwa mwanamapinduzi wa Marekani Kusini aliyeuliwa na majasusi wa Marekani (CIA) na kisha kuzikwa kisirisiri.

Thomas Sankara aliyekuwa muumini wa fikra za kupigania Umoja wa Afrika au Pan Africanist mara nyingi alionekana kutopendwa na mataifa ya magharibi kutokana na fikra zake za kupinga dhuluma za wakoloni kunyonya watu wanyonge.

Mwaka 1985, Thomas Sankara alikaririwa akisema kuhusu falsafa yake kisiasa iliyokuwa maarufu, ilikuwa ikisema;

‘you cannot carry out fundamental change without a certain amount of madness’, yaani kwa tafsiri isiyo rasmi, hauwezi kuleta mageuzi ya msingi bila kuwa na kiasi fulani cha ukichaa ndiyo maana mabeberu walieneza propaganda kwamba Sankara ni kichaa anayeingoza Burkina Fasso.

Pamoja na yote na mengi mazuri, wapinzani ndani na nje ya nchi ya Burkinafasso, walisikika wakimlaumu Sankara kwa kupiga marufuku vyama huru vya wafanyakazi na vyama vya siasa.

Pia Sankara alianzisha Mahakama za wananchi ‘people’s revoluntionary tribunals’ ambazo zililenga kutoa hukumu kwa wapinga mapinduzi, wafanyakazi wazembe Jambo ambalo lilileta hamasa ya watumishi wa umma kufanya kazi kwa nguvu wakiogopa hukumu.

Ila hatua hiyo ilipigwa vita saba na wapinzani wake.

Kumbukumbu kubwa ya wananchi wa Burkinabe (Burkina fasso), kuhusu Kapteni Thomas Sankara, ilikuwa ni wiki moja kabla ya kuuwawa kwake alitabiri, na alikaririwa akisema:

“Wanamapinduzi wanaweza kuuliwa, lakini fikra za kimapinduzi zitaendelea kuishi daima”

Hapo alikuwa akinukuu maneno ya Mwanamapinduzi maarufu Duniani, Ernesto Che Guevara ambaye aliwahi kusema..

“Revolutionaries and individuals can be murdered, but ideas never die.”

Thomas Sankara alifariki Oktoba 15 mwaka 1987 baada ya kupinduliwa na Blaise Compaore kuchukuwa utawala nchini Burkina Faso kwa muda wa miaka 27.

Inafahamika kwamba, kwa mara ya kwanza mwaka 1997, familia ya marehemu Thomas Isodoré Noël Sankara, ilifikisha ombi la kutaka mwili wa Sankara ufukuliwe ili ufanyiwe uchunguzi.

Taarifa zinafahamisha kuwa serikali ya Blaise Compaore ilitupilia mbali ombi kutoka familia ya Thomas Sankara la kutaka kufanyike uchunguzi kuhusu kifo cha Sankara.

Kwa mujibu ya ripoti ya kifo cha Thomas Sankara, serikali ilifahamaisha kuwa Thomas Sankara alifariki kifo cha kawaida.

Familia ilitaka kufahamu kama ni kweli katika kaburi hilo ndipo mwili wa Thomas Sankara ulipohifadhiwa.
375adb3906bcf3759f3cc96788dbc7e8.jpg
71fecd849c75de6a217f18e63385dd3b.jpg
b18af6adb7427961ce7241627de7bfa0.jpg




Sent from my TECNO H5 using JamiiForums mobile app
 
“Huwezi kufanya mabadiliko ya msingi pasipo na kiasi fulani cha uwendazimu. Katika hali hiyo, inaendana na kutofungamana na upande wowote, ujasiri wa kuweza kuzipa mgongo taratibu zilizopita, ujasiri wa kuivumbua kesho yenu. Iliwachukua wendawazimu waliopita kabla yetu kwa sisi kuwa na walau kiasi cha ujasiri tulionao leo. Ninataka niwe mmoja wa wendawazimu hao. Ni lazima tuthubutu kuivumbua kesho yetu.”

Thomas Sankara
Rais wa Burkina Faso
(4 August 1983 – 15 October 1987)

FB_IMG_1505763941596.jpg
 
Uliza kilichomtokea!!!!
Nyerere hakuwahi hata kumpa barabara ya jina lake Dar.
Uwendawazimu kama Mtu flani bila staha wala utu wala ubinadamu!!! Lazima mwisho wako utakuwa mbaya.
RIP Sankara!!!!
Sijakuelewa mkuu,unamaanisha sankara alikua muuaji ? Mbn ndo naskia kwako,kwa ninavojua huyu jamaa alikua peace sana
 
Uliza kilichomtokea!!!!
Nyerere hakuwahi hata kumpa barabara ya jina lake Dar.
Uwendawazimu kama Mtu flani bila staha wala utu wala ubinadamu!!! Lazima mwisho wako utakuwa mbaya.
RIP Sankara!!!!
Hakika huijui historia ya Sankara.
Fanya tafiti huwa zinasaidia kuliko mihemko ya kisiasa. Watu weupe walituletea mifumo ya siasa Afrika ili waendelee kututawala kifikra na Maendeleo. Wakavuruga taratibu zetu za kiAfrika...ilhali wao mpaka leo hii wanaheshimu ufalme (monarchy) japokuwa wana vyama vya siasa.
Viongozi wa nchi za Afrika waliokuwa na maono na fikra za kuwakomboa Waafrika na bara la Afrika kwa ujumla walionekana ni tishio kwa wakoloni na Wezi wa rasilimali zetu.
Nenda kasome historia ya Sankara itakusaidia kuondoa hizo fikra chafu ulizopandikizwa na makaburu.

Tafuta kitabu chake kinaitwa " Thomas Sankara Speaks". Ukisome na ukielewe. Itakusaidia kufungua akili yako.
 
Uliza kilichomtokea!!!!
Nyerere hakuwahi hata kumpa barabara ya jina lake Dar.
Uwendawazimu kama Mtu flani bila staha wala utu wala ubinadamu!!! Lazima mwisho wako utakuwa mbaya.
RIP Sankara!!!!
Nadhani jambo jema tukujue wewe ni nani.. uko wapi na lengo lako hasa ni lipi sabbu maneno yako hapo juu yanabeba dhamira kuu uliyo nayo ndani yako...
 
Back
Top Bottom