Tyrone Kaijage
JF-Expert Member
- Jul 19, 2021
- 1,617
- 3,405
Thomas Sankara na Blaise Compaoré, wote walikua pamoja nyumbani kwetu. Baba yangu aliwatunza wote wawili na walikuwa zaidi ya ndugu. Baba yangu aliwapeleka wote wawili kwa jeshi la taifa na kuhakikisha kwamba wote wameandikishwa.
Walipopata habari katika familia yetu kwamba kaka yangu amepinduliwa na kuuawa na Blaise Compaoré, ilikuwa wakati wa huzuni zaidi katika maisha ya familia yetu lakini baba yangu alikuwa thabiti, alisema, wanandugu kutoelewana hutokea. Kisha akatuma wajumbe kwa Blaise arudi nyumbani na kuketi naye ili kumweleza kilichotokea, alikuwa tayari kumsamehe na kumrudisha kama mtoto wake kama ambavyo amekuwa siku zote.
Lakini, baba yangu alingoja hadi kifo chake bila kupata fursa ya kujua ni nini hasa kilimpata Thomas au kumsamehe Blaise Compaoré kwa sababu hakurudi nyumbani kwetu tena."
-Odile Sankara (Dada yake na Thomas Sankara)