Thomas Sankara na Blaise Compaore

Thomas Sankara na Blaise Compaore

Tyrone Kaijage

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
1,617
Reaction score
3,405
Thomas Sankara na Blaise Compaoré, wote walikua pamoja nyumbani kwetu. Baba yangu aliwatunza wote wawili na walikuwa zaidi ya ndugu. Baba yangu aliwapeleka wote wawili kwa jeshi la taifa na kuhakikisha kwamba wote wameandikishwa.

Walipopata habari katika familia yetu kwamba kaka yangu amepinduliwa na kuuawa na Blaise Compaoré, ilikuwa wakati wa huzuni zaidi katika maisha ya familia yetu lakini baba yangu alikuwa thabiti, alisema, wanandugu kutoelewana hutokea. Kisha akatuma wajumbe kwa Blaise arudi nyumbani na kuketi naye ili kumweleza kilichotokea, alikuwa tayari kumsamehe na kumrudisha kama mtoto wake kama ambavyo amekuwa siku zote.

Lakini, baba yangu alingoja hadi kifo chake bila kupata fursa ya kujua ni nini hasa kilimpata Thomas au kumsamehe Blaise Compaoré kwa sababu hakurudi nyumbani kwetu tena."

-Odile Sankara (Dada yake na Thomas Sankara)
 
Compaore angemuomba Sankara kama yeye anataka Urais mbona angepewa utaratibu tu hata wa baada ya muda na yeye kuwa Rais kuliko kumtoa uhai mshikaji wake wa karibu kwa urafi tu wa madaraka.
 
Blaise alikua mshenzi tu. Kila binadamu anazalliwa na roho yake. Pamoja na kulelewa pamoja watu hawa wawili walikua na tabia tofauti kabisa

Nimewahi kukutana na Bi Mariam Sankara Dubai na anaelezea stori ya marehemu mumewe na huyo “ndugu yake” Compaore katika hali ya mshangao kama vile matukio hayo yametokea jana tu
 
Thomas Sankara na Blaise Compaoré, wote walikua pamoja nyumbani kwetu. Baba yangu aliwatunza wote wawili na walikuwa zaidi ya ndugu. Baba yangu aliwapeleka wote wawili kwa jeshi la taifa na kuhakikisha kwamba wote wameandikishwa. Walipopata habari katika familia yetu kwamba kaka yangu amepinduliwa na kuuawa na Blaise Compaoré, ilikuwa wakati wa huzuni zaidi katika maisha ya familia yetu lakini baba yangu alikuwa thabiti, alisema, wanandugu kutoelewana hutokea. Kisha akatuma wajumbe kwa Blaise arudi nyumbani na kuketi naye ili kumweleza kilichotokea, alikuwa tayari kumsamehe na kumrudisha kama mtoto wake kama ambavyo amekuwa siku zote. Lakini, baba yangu alingoja hadi kifo chake bila kupata fursa ya kujua ni nini hasa kilimpata Thomas au kumsamehe Blaise Compaoré kwa sababu hakurudi nyumbani kwetu tena." -Odile Sankara (Dada yake na Thomas Sankara)
Urafiki/undugu wa mashtaka !
 
Hizi ni historia za kuzizingatia sana hasa kwa kikazi hiki cha kuwana machawa na marafiki wakukuona unapata tuu.
 
Katika watu ninaowachukia dunia hii ni huyo hayawani anaitwa Blaisie Compaore. Lakini malipo ni hapa hapa duniani, si mnaona alivyofukuzwa kama fisi toka Ikulu nusura wampasue kibofu. Sasa anakabiliwa na mashitaka ya kumuua Tom Sankara. Natamani arudishwe toka huko aliko, aje akumbane na kesi yake, akutwe na hatia, ahukumiwe kunyongwa (kama hukumu hiyo ipo huko) kisha hukumu itekelezwe! Bazazi mkubwa na mjaa laaana.
 
Mzee alifuga nyoka...

Thomas..alikuwa cool sana na alipendwa na raia mno tofauti na iblis compare..
Kamuua mwenziwe huku anamtizama ...
 
Back
Top Bottom