Thomas ulimwengu atimka TP Mazembe rasmi

Mr Hero

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2015
Posts
5,540
Reaction score
7,455
thomas-ulimwengu.jpg

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu ameachana na klabu yake ya TP Mazembe ya nchini Congo DR baada ya kumalizika kwa mkataba wake.

Ulimwengu ambaye ameitumikia Mazembe kwa miaka mitano, ameamua kufatilia ofa mbalimbali za vilabu vya barani Ulaya.

Licha ya TP Mazembe kufanya juhudi za kutaka kumpaka mkataba mpya, Ulimwengu hakuwa tayari badala yake akasisitiza kuwa, ni muda muafaka kwake kufuata nyayo za Mbwana Samatta kwenda kucheza soka la kulipwa bara la Ulaya.
 
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu ameachana na klabu yake ya TP Mazembe ya nchini Congo DR baada ya kumalizika kwa mkataba wake.

Ulimwengu ambaye ameitumikia Mazembe kwa miaka mitano, ameamua kufatilia ofa mbalimbali za vilabu vya barani Ulaya.

Lich ya TP Mazembe kufanya juhudi za kutaka kumpaka mkataba mpya, Ulimwengu hakuwa tayari badala yake akasisitiza kuwa, ni muda muafaka kwake kufuata nyayo za Mbwana Samatta kwenda kucheza soka la kulipwa bara la Ulaya.
Atakuwa alikuwa expendable kwa Moise Katumbi, mpaka mkataba unaisha? Mbona Samata jasho lilimtoka katumbi!
 
Kwa kipaji kurudi kucheza klabu yoyote bongo hapana, aje achezee Taifa Stars tu!
 
Mkuu nimesema kwa muda anaosubiria timu, siyo kwa muda anausubiri dirisha.
Akija simba itabidi asajiliwe ili acheze, na akishasajiliwa akishapata hiyo timu itambidi asubiri dirisha lifunguliwe jan,
Alafu mbona kashasema ana ofa tatu ndio anachagua ipi itakayomfaa, mabingwa wa africa wanamtaka ila kaipotezea anataka aende ufaransa au ubelgiji ndio anafikiria afanye uamuzi
 
Sure sure, tumwombee apate timu fasta. Kuwa free agent ni kipindi kigumu sana kwa mchezaji.
 
Akija simba itabidi asajiliwe ili acheze, na akishasajiliwa akishapata hiyo timu itambidi asubiri dirisha lifunguliwe jan,
Alafu mbona kashasema ana ofa tatu ndio anachagua ipi itakayomfaa, mabingwa wa africa wanamtaka ila kaipotezea anataka aende ufaransa au ubelgiji ndio anafikiria afanye uamuzi
Hapa ndo pa kumpa ushauri
 
Ametimka kwani msimu rasmi Wa ligi huko Congo umemalizika!? Kama amekataa kusaini mkataba mpya ni wazi ataendelea kucheza mpaka ligi inapoisha huku akiendelea kuzungumza na timu nyingine.
 
Anataka kwenda Ulaya we unamshauri aje Majungu FC. Simba na Yanga nyie wote longolongo tu.
Simba huwa haimbanii mchezaji mikataba ya wachezaji Wa simva iko wazi wakipata timu nje tofauti na Vyura fc aka mbeleko fc
 
Back
Top Bottom