Mr Hero
JF-Expert Member
- Jun 11, 2015
- 5,540
- 7,455
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu ameachana na klabu yake ya TP Mazembe ya nchini Congo DR baada ya kumalizika kwa mkataba wake.
Ulimwengu ambaye ameitumikia Mazembe kwa miaka mitano, ameamua kufatilia ofa mbalimbali za vilabu vya barani Ulaya.
Licha ya TP Mazembe kufanya juhudi za kutaka kumpaka mkataba mpya, Ulimwengu hakuwa tayari badala yake akasisitiza kuwa, ni muda muafaka kwake kufuata nyayo za Mbwana Samatta kwenda kucheza soka la kulipwa bara la Ulaya.