THRDC, EAHRI na DPI watoa Mafunzo kuhusu Utakatishaji Fedha na Njia zinazotumika Kufadhili Ugaidi kupitia Asasi za Kiraia

THRDC, EAHRI na DPI watoa Mafunzo kuhusu Utakatishaji Fedha na Njia zinazotumika Kufadhili Ugaidi kupitia Asasi za Kiraia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
IMG_2130.JPG
GMTL5388.jpg
GMTL5397.jpg

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), kwa kushirikiana na Taasisi ya Haki za Binadamu Afrika Mashariki (EAHRI) na Shirika Lisilo la Kiserikali Defenders Protection InternationaI (DPI) lenye Makao yake Nchini Uganda wameendesha Mafunzo ya Siku 2 yanakayofanyika Dar es salaam kati ya Machi 12, 2023 na Machi 14, 2023.
gmtl5389-jpg.2548733

Malengo ya Mafunzo yanajumuishwa katika malengo makuu ambayo ni:

1. Kuzifahamisha Asasi za Kiraia na Mashirika yasiyo ya kiserikali nini maana ya Utakatishaji Fedha, Njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika kutakatisha Fedha kupitia Asasi za Kiraia na Mashirika yasiyo ya Kiserikali na fedha ambazo zinapatikana na kutumika kufadhili ugaidi, na jinsi gani utakatishaji Fedha unatokea.

2. Jinsi gani Serikali kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia na Mashirika yasiyo ya kisirikali zinaweza kutokomeza kabisa utakatishaji fedha nchini Tanzania na ufadhili wa mipango ya kigaidi.

3. Kuzijengea uwezo asasi za kiraia jinsi ya kuepukana na fedha na mali zilizopatikana kwa njia haramu na zenye lengo la kufanyiwa utakatishaji au kufadhili ugaidi.

4. Kuwajengea uwezo AZAKI/Watetezi wa Haki za Binadamu juu ya Sera, Sheria na Mikakati inayoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Tanzania ili kupambana na Utakatishaji Fedha na Ufadhili wa Ugaidi hasa kwa upande wa Mashirika yanayofanya kazi bila faida (NPOs/AZAKI).

5. Kuhakikisha mikakati hii mizuri ya kupambana na utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi haitumiki vibaya kwa malengo yasiyo rasmi kudidimiza nafasi za kiraia nchini ( Civic Space) Washiriki kwenye mafunzo haya ni wawakilishi toka ofisi za wasajili wa AZAKI nchini (kutoka Ofisi ya Msajili NGOs, Msajili wa Societies kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani na Msaji kutoka RITA) na Mrajis wa AZAKI kutoka Zanzibar.
gmtl5383-jpg.2548728

Wengine ni wataalam toka Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya ndani (Ikiwemo Idara Maalum ya kudhibiti Fedha Haramu -FIU), Baraza la NGOs (NACONGO), Asasi za Kiraia ikiwemo JAMII FORUMS, na Watetezi wa Haki za Binadamu.

Asasi za Kiraia ni wadau muhimu katika mafunzo haya sababu wako katika hatari kubwa ya kushiriki katika utakatishaji wa fedha na Ugaidi kwa kujua ama kutokujua. Hii ni kwa sababu kazi nyingi zinategemea wafadhili ambao mara nyingi ni kutoka ughaibuni na ambao kwa kiasi fulani huwa ni vigumu kufahamu vyanzo vyao vya fedha ambazo hutumika kufadhili mashirika yasiyo ya kiserikali katika kutimiza miradi yao mbalimbali.

Asasi za Kiraia zinahitaji mafunzo haya ili zipate mbinu na uwezo kuisaidia Serikali na wao binafsi kupambana na kujikinga kushutumiwa kujihusisha na utakitshaji wa fedha na fedha zinazopatikana kwa njia za kigaidi au zinazofadhili ugaidi aidha kwa kujua au kutokujua.

Mafunzo haya yatakuwa endelevu na yatakuwa yakitolewa kwa kanda zote 11 za THRDC ili kuwafikia wadau wengi zaidi. Lengo ni kuhakikisha tunashirikiana na serikali katika kufikia malengo yanayotakiwa katika kutokomeza mazingiria ya viashiria vyote vya utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi. Ikumbukwe Tanzania ni Mwananchama wa Kamati Maalum (Financial Task Force -FATF) yenye majukumu ya kupambana na swala hili.
gmtl5390-jpg.2548734

gmtl5391-jpg.2548735

gmtl5399-jpg.2548741

gmtl5401-jpg.2548743

gmtl5404-jpg.2548745

gmtl5406-jpg.2548746

gmtl5414-jpg.2548752

IMG_2130.JPG
 

Attachments

Back
Top Bottom