THRDC: Kukamatwa kwa viongozi, wafuasi wa Chadema kuna lenga kuwazuia kufanya shughuli ya maadhimisho ya vijana duniani

THRDC: Kukamatwa kwa viongozi, wafuasi wa Chadema kuna lenga kuwazuia kufanya shughuli ya maadhimisho ya vijana duniani

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania(THRDC) umelaani vitendo vya kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA, akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho bara, Tundu Lissu, Katibu Mkuu John Myika,Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi, Wakili Deogratias Mahinyila, baadhi ya viongozi wa BAVICHA, pamoja na Wanahabari.

Kufuatia kukamatwa kwa viongozi pamoja na watu hao katika maeneo tofauti, Mtandao umetoa wito kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini kuwaachilia huru watu wote waliokamatwa bila masharti ili waweze kuadhimisha siku ya vijana duniani ambayo ilipangwa kufanyika leo.

Soma Pia:
"Ibara ya 18 na 20(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinatoa haki na uhuru wa watu kujumuika, kufanya mikutano, maadhimisho na kueleza mawazo yao. Haki hizi hazipo kwenye Katiba peke yake bali zipo kwenye Mikataba mbalimbali ya Kimataifa na
Kikanda ambayo Tanzania imeridhia." imeelezwa katika tamko hilo
Screenshot_20240812-083415_1.jpg

Screenshot_20240812-083423_1.jpg
 
Yaliyotokea Kenya yalianza na kadhia ndogondogo kama hizi. Hasira ikiwajaa wanaingia barabarani na hapo ndio nguvu ya Umma huonekana.

Polisi wetu hawajawahi kuingia majaribuni ya maandamani makubwa naona kama wanawashawishi watu kuingia barabarani.
 
Back
Top Bottom