Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),Wakili Onesmo Olengurumwa amesema kuwa wamesikitishwa na tukio la kukamatwa kwa viongozi wa CHADEMA leo Aprili 24, 2025, wakati wakielekea Mahakama ya Kisutu kushiriki usikilizaji wa kesi ya Mwenyekiti wao Tundu Antiphas Lissu.
Amesema wanatoa wito kwa Serikali kupitia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), na vyombo vya sheria kuhakikisha Taifa linaendelea kulinda misingi ya demokrasia na kuzingatia majadiliano kama njia ya kutatua tofauti za kisiasa.
Video: Watetezi tv (YouTube)
View: https://youtu.be/u-wbF_Y4d3E?si=S6jJX1cWXxlSc_k7
Olengurumwa amesema ni jambo la kusikitisha kuona matumizi ya nguvu yakichukua nafasi katika mazingira ya kisiasa.
“Ni muhimu sana Serikali ikasikiliza sauti ya upinzani kwa njia ya mazungumzo, matumizi ya nguvu hayawezi kutuletea mshikamano wa kitaifa,” amesema.
Mapema leo iliripotiwa viongozi waandamizi wa CHADEMA akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Bara John Heche na Katibu Mkuu John Mnyika kukamatwa na polisi katika eneo la Daraja la Salenda, wakielekea Mahakama ya Kisutu.
Itakumbukwa hivi karibuni baada ya Tundu Lissu kukamatwa na kufunguliwa kesi THRDC taarifa ya wito kwa mamlaka kumuachia mshtakiwa huyo anayekabiliwa na kesi ya uhaini, lakini pia walitoa ushauri kwa kuwepo kwa 'muafaka wa kitaifa' ambao umbao utajikita kutafuta suluhu ya changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wadau wa demokrasia nchini hususani kipindi cha uchaguzi.
www.jamiiforums.com

PreGE2025 - THRDC: Tumesikitishwa na kukamatwa kwa Lissu na kufunguliwa kesi ya uhaini, DPP aondoe shtaka hilo Mahakamani
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umesikitishwa na kukamatwa na kufunguliwa kesi ya uhaini, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu, ambapo wametoa wito kwa mwendesha mashtaka kuondoa kesi hiyo au kubadili hati ya mashtaka ili kumuwezesha kuachiliwa kwa dhamana...
PreGE2025 - THRDC yapendekeza mambo 10 ya muafaka wa Kitaifa kufanikisha Uchaguzi wa Amani
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umetoa wito wa kupatikana kwa Muafaka wa Kitaifa utakaoliwezesha taifa kuelekea kwenye uchaguzi kwa umoja, utulivu na mshikamano. Kwa mujibu wa THRDC, muafaka huo ni muhimu kwani utatoa fursa ya kushughulikia changamoto na dukuduku...