Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) imetoa mapendekezo kwa Serikali kutumia mamlaka ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuangalia uwezekano wa kuondoa mahakamani kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ili kutoa nafasi ya mazungumzo na maridhiano nchini.
Uhuru wa Habari na Watetezi wa Haki: Kuhakikisha uhuru wa waandishi wa habari, watetezi wa haki za binadamu, na wadau wengine wanaofuatilia mwenendo wa kesi hiyo ili waweze kutekeleza wajibu wao bila kuingiliwa.
Uchunguzi wa Tuhuma za Muteso: Kufanya uchunguzi wa haraka, huru na wa ufanisi kuhusu tuhuma zote za kushambuliwa, kuteswa, kutishwa na kutendewa vibaya kwa watu wowote wanaohusishwa na mwenendo wa kesi hiyo au uwajibikaji wao.
Matumizi ya Mamlaka ya DPP: Kutumia mifumo halali ya kisheria kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ili kuondoa shauri la Tundu Lissu mahakamani pale inapofaa kwa mujibu wa sheria.
Fursa ya Mazungumzo: Kutoa nafasi ya mazungumzo na maridhiano baina ya makundi mbalimbali ya kijamii, ikiwa ni pamoja na kumhusisha Tundu Lissu na chama chake cha CHADEMA ili kurejesha mshikamano wa kitaifa.
THRDC imesisitiza kuwa matumizi ya njia za kisheria na mazungumzo ndiyo msingi mkuu wa kupata suluhisho la kudumu litakalolinda haki za binadamu na kuimarisha amani nchini.
Katika tamko hilo, THRDC imetoa mapendekezo kuu nne kwa Serikali:Uhuru wa Habari na Watetezi wa Haki: Kuhakikisha uhuru wa waandishi wa habari, watetezi wa haki za binadamu, na wadau wengine wanaofuatilia mwenendo wa kesi hiyo ili waweze kutekeleza wajibu wao bila kuingiliwa.