Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeeleza wasiwasi wake kuhusu kukamatwa kwa wahadhiri watatu wa vyuo vikuu, huku mmoja wao akifunguliwa kesi ya ugaidi na wengine wawili wakiendelea kushikiliwa bila maelezo. Umesema hali hiyo inaweza kuwa na athari kwa taaluma na kuathiri ubora wa elimu ya juu pamoja na maendeleo ya utafiti nchini.
Katika tamko lililotolewa Julai 30, 2026, na Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa, imesisitizwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria, wakiwemo wahadhiri, watafiti na wanazuoni. Hata hivyo, imeelezwa kuwa kuwakamata katika mazingira yanayohusisha utekelezaji wa majukumu yao ya kitaaluma kunaongeza hofu na kupunguza uhuru wa wanataaluma.
THRDC imesema kuwa mafundisho ya darasani, uchambuzi wa kitaaluma, mijadala ya kisheria au ukosoaji wa sera za umma haviwezi kuwa msingi wa mashtaka ya ugaidi bila ushahidi unaokidhi matakwa ya sheria.
Kwa mujibu wa THRDC, wahadhiri watatu waliokamatwa mwezi Julai mwaka huu ni pamoja na Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Melkisedeki Kitunzi Kaijage; Bw. Johaiven Revelian Bikongolo wa Chuo Kikuu cha St. John kilichopo Dodoma; na Bw. Titus Joseph Kituli wa chuo hicho.
THRDC imesema kuwa wahadhiri hao wawili wa Chuo Kikuu cha St. John bado wanaendelea kushikiliwa bila kufikishwa mahakamani wala kuelezwa wazi tuhuma zinazowakabili. Imeeleza kuwa hali hiyo inaendelea kuibua hofu kwa wanataaluma nchini.
"Kukamatwa kwa wahadhiri hivi karibuni, ikiwemo kufunguliwa kwa shtaka linalohusiana na ugaidi, kumeibua wasiwasi ndani ya jumuiya ya kitaaluma. Kushikiliwa kwa muda mrefu, kubadilika kwa maelezo ya tuhuma na kutumia mashtaka yasiyo na dhamana dhidi ya wanataaluma kunaweza kuwafanya wengine waone kuwa ufundishaji, utafiti au ushiriki halali katika masuala ya umma unaweza kuwaweka katika hatari ya uchunguzi au mashtaka yasiyo na dhamana," THRDC imeeleza.
Kufuatia hali hiyo, THRDC imetoa wito kwa Jeshi la Polisi Tanzania kuweka wazi tuhuma dhidi ya Bw. Johaiven Revelian Bikongolo na Bw. Titus Joseph Kituli, kuwaachia kwa dhamana ya polisi au kuwafikisha mara moja mbele ya mahakama yenye mamlaka, na kuhakikisha wanapata huduma za wakili pamoja na fursa ya kuwasiliana na familia zao.
Pamoja na wito huo, THRDC imesisitiza kuwa ni vyema mamlaka za uchunguzi na mashtaka kutotumia Sheria ya Kuzuia Ugaidi au sheria nyingine za jinai dhidi ya ukosoaji au mijadala ya kitaaluma inayokidhi misingi ya sheria.
Pia, THRDC imetoa wito kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania na mamlaka za vyuo vikuu kuandaa na kutekeleza sera za kulinda uhuru wa kitaaluma na uhuru wa kujieleza; kutoa msaada kwa wahadhiri na wanafunzi wanaokabiliwa na hatua za kisheria kutokana na kazi halali za kitaaluma; na kuweka taratibu za kushughulikia ufuatiliaji wa siri, uingiaji holela wa vyombo vya dola pamoja na ukamataji unaofanyika ndani ya vyuo vikuu.