THRDC: Watatu wanaoshikiliwa kwa kupanga maandamano kwenye mkutano wa IPU waachiliwe huru

THRDC: Watatu wanaoshikiliwa kwa kupanga maandamano kwenye mkutano wa IPU waachiliwe huru

informer 06

Senior Member
Joined
May 11, 2024
Posts
184
Reaction score
170
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umesema umesikitishwa na taarifa za kukamatwa kwa wafanyakazi watatu wa Baraza la Wanawake Wafugaji (PWC), shirika lisilo la kiserikali linalofanya shughuli zake jijini Arusha.

IMG_3495.jpeg

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na THRDC, Oktoba 6,2026, Polisi waliwakamata wafanyakazi wa PWC, Thadeus Clamian, Nangei Meitaya na Ezekiel Kishau, pamoja na Salangat Makko ambaye, kwa mujibu wa taarita hiyo, si mfanyakazi wa PWC.

THRDC imesema imepokea taarifa kwamba watu hao wanatuhumiwa kupanga maandamano yanayohusishwa na wabunge wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Mtandao huo pia umedai kuwa Polisi wanaendelea kuwatafuta wafanyakazi wengine wa PWC, huku baadhi yao
wakifuatiliwa hadi majumbani kwao nyakati tofauti, ikiwemo usiku.

Aidha, THRDC imesema Oktoba 5, 2026, Polisi walifanya upekuzi katika moja ya makazi ya mfanyakazi wa PWC wakati wa usiku, bila kutoa maelezo ya sababu za upekuzi huo.

Kwa mujibu wa THRDC, hali hiyo imesababisha hofu na wasiwasi miongoni mwa wafanyakazi wa PWC, familia zao pamoja na mashirika ya kiraia jijini Arusha.

Katika hatua nyingine, THRDC imesema imewaelekeza Mawakili Simon Mbwambo na Ally Mhyellah kufuatilia suala hilo katika Kituo cha Polisi Kati, Arusha, kwa ajili ya kutoa msaada wa kisheria kwa waliokamatwa. Wakili Lairumbe pia anaendelea kufuatilia suala hilo kwa niaba ya PWC.

THRDC imezitaka mamlaka za Polisi kuwaachia wafanyakazi hao bila masharti, ikisema hakuna shirika lolote mwanachama wa mtandao huo linaloratibu maandamano hayo.

Aidha, imetaka wafanyakazi wote waliokamatwa wapewe fursa ya kuwasiliana na mawakili wao pamoja na familia zao.

Taarifa hiyo imetolewa na Mratibu wa THRDC Wakili Onesmo Olengurumwa
 
Back
Top Bottom