THRDC Yalaani Polisi Kuwashikilia Waandishi wa Habari Arusha Zaidi ya Saa 24 Bila Dhamana

THRDC Yalaani Polisi Kuwashikilia Waandishi wa Habari Arusha Zaidi ya Saa 24 Bila Dhamana

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umelaani vikali Suala la Jeshi la Polisi kuwashikilia kwa zaidi ya saa 24 waandishi wawili wa habari Arusha, bila kuwapa dhamana. Waandishi hao ni Baraka Lucas wa Jambo TV na Ezekiel Mollel wa Manara TV, ambao walikamatwa Septemba 6, 2025, wakituhumiwa kuendesha televisheni mtandaoni bila leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 10, 2025, Mratibu Kitaifa wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa, amesema kuwa kuwashikilia waandishi hao kwa zaidi ya saa 24 bila kuwapa dhamana wakati makosa yao yanadhamika ni ukiukaji wa sheria za nchi.

Soma Pia: Polisi: Waandishi wa Habari wa Jambo TV na Manara TV wamekamatwa kwa Kuendesha Online TV Zisizosajiliwa

Olengurumwa ameendelea kufafanua kuwa, mtu yoyote anayefikishwa kituo cha polisi ana haki ya kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili, na hatua ya kushikilia waandishi bila kufuata taratibu hizo ni kinyume na misingi ya haki za binadamu na utawala wa sheria.

THRDC imezitaka mamlaka husika kuhakikisha wanahabari wanapata haki zao zote za kimsingi na bila kukiuka taratibu za kisheria.
 
Back
Top Bottom