PreGE2025 POTOSHI THRDC yatoa tamko kukemea unyanyasaji dhidi ya Tundu Lissu ikidai kufanywa na mawakili wake

PreGE2025 POTOSHI THRDC yatoa tamko kukemea unyanyasaji dhidi ya Tundu Lissu ikidai kufanywa na mawakili wake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
IMG_1063.JPG

IMG_1064.JPG
 
Tunachokijua
THRDC ni muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania ambao ulianzishwa mwaka 2010 katika kipindi ambacho matukio ya uvunjaji wa haki za binadamu yalikuwa juu kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania.

Muungano huo unafanya kazi ya kuboresha usalama na ulinzi wa watetezi wa haki za binadamu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuhakikisha kuwa watetezi wa haki za binadamu wanaweza kutekeleza majukumu yao muhimu bila hofu ya madhara au ukandamizaji, kwa mujibu wa Azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1998 kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu.

Mnamo mwezi Aprili 24, 2025 Lissu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kukamatwa Aprili 09, 2025 mkoani Ruvuma, na kusomewa mashitaka matatu ikiwemo uhaini na kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa X ambapo kesi hiyo ilihairishwa hadi Mei 06, 2025.

Aidha Mei 03, 2025 Jopo la mawakili wanaomtetea Lissu walifanya mkutano na waandishi wa habari wakiongozwa na wakili Peter Kibatala ambapo alisema wameamua kuzungumza na waandishi wa habari ili kuwaeleza watanzania uhalisia wa masuala mbalimbali kuhusu kesi hiyo.

Madai
Kumeibuka taarifa inayodaiwa kutolewa na THRDC na kuchapishwa na Watetezi TV kuwa wametoa tamko la kukemea kile kilichodaiwa kuwa unyanyasaji dhidi ya Tundu Lissu unaofanywa na mawakili wake.

Uhalisia
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key Word Search) umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli, imetengenezwa na wapotoshaji kwani haijachapishwa katika kurasa za THRDC na Watetezi TV.

Aidha madai hayo si ya kweli kwani katika mkutano na waandishi wa habari Wakili Kibatala alieleza nia ya mteja wao Tundu Lissu kutaka kususia kula chakula ili kushinikiza kutendeka kwa haki katika uendeshaji wa kesi inayomkabili. Hivyo taarifa zinazodai kuwa Lissu anashinikizwa na mawakili wake kususia chakula si ya kweli bali ni taarifa zenye lengo la kupotosha uhalisia.

"Natoa taarifa rasmi kwa umma kwa niaba ya mteja wetu kwamba anfanya 'hunger strike' anaanza kususia kula chakula, sio kwa sababu nyingine, anataka haki itendeke. Kwahiyo Antipas Tundu Lissu Mughwai kwa siku ambayo ataamua, tutatoa taarifa fupi hasa kuhusu siku lakini taarifa ni hiyo kwamba atasusa kula chakula, kitakachomtokea yuko tayari, hatakula chakula mpaka pale atakapoona haki inatendeka"

Rejea hapa kuanzia 1:18:39

View: https://www.youtube.com/live/5xlvQC3UEMo?si=hjnifpE7DY0uD5E1&t=4714​
Back
Top Bottom