Thread maalum kukumbushana michezo ya utotoni iliyosahaulika

Hii tuliita anagusha bwege,

Tobo dunda, hii tunacheza mpira ukikupita tobo tunaanza kukudunda ,unapigwa mpaka ujiokoe

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Miaka ya 90 katika mchezo wa Mpira wa miguu mtaani kulikuwa na .....

Gombania goli ,

magoli madogo,

timu kutoka,

penalty-penalty

Danadana.

Mstari kati
hyo gombania goli Mtu akifunga basi anachagua mchezaji wa kukaa nje.. kuna watu walikua wakifunga tu wakwanza kutoka nje mm πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Sisi wengine hatukupata nafasi ya kucheza kabisa.
Wewe utakuwa wa kishua!

Watu tumecheza hadi style za doggy na mbuzi kagoma tukidhani sisi ndo wagunduzi!

Enzi hizo tuliamini kugegedana ni mchezo wa watoto, tulipokua ndo tukagundua kumbe ni mchezo wa wakubwa, na mbaya zaidi ndo uliotuleta duniani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoano .Mnakuwa watoto wengi kwenye kiwanja ili wote mcheze mpira mnachaguana kwa idadi fulani ,team ikipigwa kamba mbili nje inaingia nyingine.Namkumbuka sana mwanangu Mashimila bonge moja la striker kidato cha nne tu akalamba ajira 82 rangers.Mimi hapo playmaker kama Shinji Kagawa nagusa mara moja tu.Nikarogwa goti ,nikajikita kwenye shule tu.
 
Mchezaji: Namsaka mke wangu, namsaka mke wangu!

Wote: Hapa hayupo hapa hayupo.

Mchezaji: Kaenda wapi, kaenda wapi?

Wote: Kaenda kusuka, kaenda kusuka.

Mchezaji: Kachukua nini na nini?

Wote: Kachukua chanuo na mafuta...

Huu mti gani?

Wa mchongoma...

Nikiukata?

Haukatiki...

Kwa panga?

Haukatiki...

Kwa Shoka?

Haukatiki....

Huu mchezo uliwaandaa wasichana kukingiana vifua kwenye mishe zao tu.
[emoji16]
 
Tulikwenda (Na Mimi)
Mlimani (Na Mimi)
Tukamkita (Na Mimi)
Sungura (Na Mimi)
Anafana (Na Mimi)

Basi utacheeeeeekwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…