Eng. Zezudu
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 8,024
- 11,546
Hii tuliita anagusha bwege,Mpira wa utotoni miaka ya 80s na 90s na 2000s (2000-2005) mwanzoni mambo yalikuwa supa.
Sijui nani alikuwa analeta mbinu(tactics) za kuujua na kuelewa vizuri mpira wa miguu ili mchezaji kuwa bora zaidi.
Nimekumbuka hii michezo;
1. SAFA(suffer) BWEGE
Hapa wachezaji mnakuwa kwenye mpagilio wa mzunguko(round) kisha mchezaji mmoja (BWEGE) anaingia kati na kutafuta mpira mpaka aupate.
Anayeupoteza kwa BWEGE ndiye ataingia kati na kuchezeshwa yeye kama BWEGE. Maana wachezaji wengine wanapasiana mpira wakiwa kwenye ule mzunguko wakati BWEGE [emoji2957] anautafuta ili auguse tu mpira [emoji460].
Mara nyingine BWEGE alikuwa anakimbiza mpaka anakata tamaa [emoji43] maana kuna wachezaji walikuwa na chenga za maudhi kabla ya kutoa pasi. Ukiwa BWEGE na hautumii akili utapigwa tobo au kanzu na kisha kusindikizwa na kofi la mgongoni [emoji23].
FUNZO: Kutafuta mpira wakati ukiwa kwa wapinzani (Marking)
Endeleza unayoijua
Tobo dunda, hii tunacheza mpira ukikupita tobo tunaanza kukudunda ,unapigwa mpaka ujiokoe
Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app