Thread Maalumu kwa taarifa na tetesi za usajiri Barani Ulaya na Tanzania

Manchester united hawakomi yaliyowakuta kwa pogba!???
 
Tuna rashford, angel gomes anakuja, huyo mbalape wa nini?
 

MSHAMBULIAJI John Raphael Bocco amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Simba SC, maana yake anahitimisha miaka yake 10 ya kuichezea Azam FC.

Habari ziso na punje ya shaka ambazo zinasema kwamba yapata wiki mbili sasa tangu Bocco, maarufu kwa jina la utani kama Adebayor asaini Msimbazi.

Na kusaini kwa Bocco Simba kulifuatia kutofikia makubaliano ya mkataba mpya na timu iliyompatia umaarufu katika medani ya soka nchini, Azam FC.

Bocco alitaka dau la Sh. Milioni 40 kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kucheza Azam FC kwa mshahara ule ule wa Sh. Milioni 4, lakini uongozi chini ya Meneja, Abdul Mohammed haukukubaliana naye.


John Bocco amehitimisha miaka yake 10 ya kuichezea Azam FC kwa kusaini Simba SC

Azam ilikuwa tayari kuendelea kumlipa Sh. Milioni 4 Bocco, lakini katika upande wa dau la usajili alitakiwa kuchukua Sh. Milioni 10 na mchezaji huyo akakataa.

Kwa kuwa Simba imefanikiwa kurejea kwenye michuano ya Afrika mwakani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012 na ipo kwenye harakati za kuboresha kikosi, ikaona ni vyema kutoa Sh. Milioni 40 kumsajili mfungaji huyo bora wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Na baada ya kusaini mkataba huo, Bocco ambaye ataendelea kulipwa Sh. Milioni 4, ameingia kwenye mazoezi makali ya kujiweka fiti zaidi ili akaweze kukabiliana na changamoto ya ushindani wa namba dhidi ya washambuliaji hatari wa Simba, Muivory Coast, Frederick Blagnon, Mrundi Laudit Mavugo na mzalendo, Juma Luizio.

Kitu kimoja kizuri, Bocco anakwenda timu ambayo inafundishwa na kocha wake wa zamani, Mcameroon Joseph Marius Omog ambaye amewahi kufanya naye kazi Azam FC.

Ikumbukwe, Bocco alijiunga na Azam FC mwaka 2007 akitokea Cosmopolitan ya Dar es Salaam na akaisaidia timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake kupanda Ligi Kuu mwaka 2008 akiibuka mfungaji bora wa Daraja la Kwanza.

Baada ya hapo, Bocco akawa mshambuliaji tegemeo wa Azam FC akiiongoza kutwaa mataji kadhaa, ikiwemo Ligi Kuu mwaka 2014 na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, au Kombe la Kagame mwaka 2015.






Chanzo: binzubeiry.co.tz
 
Kama ni hivyo Boko kakosea sana, hizi timu anazokimbilia mshahara wenyewe ni utata
yaani unaweza kukaa mpaka miezi 6 hujalipwa huku ukishindilia mihogo, kwa kiwango
chako Boko umekosea sana kuikataa ofa ya AZAM.
 
simba wanaudhamini mpya so kulip mishahar sio ttzo sna..
 
Kwa muda aliohudumu ktk timu busara ingemuongoza kubaki azam ukizingatia umri ushaenda! Klabu za Simba na Yanga hazina uvumilivu endapo atachemka msimu ujao ndo itakuwa mwisho wake.
 
Ametokea club ya Ajax Amsterdam , ambako kwa mwaka mmoja aliokuwepo ameiwezesha timu hiyo kumaliza namba 2 kwenye EREDIVISIE , na ameifikisha kwenye fainali ya Europa League , ambapo walifungwa na vikongwe Man U.

Ana miaka 53 na alizaliwa nchini Uholanzi Nov 21 1963 .

Amewahi kufundisha timu za Vitesse na Maccabi Tel Aviv , anapendelea mfumo wa 4/3/3

Kila la heri Dortmund .
 
Mkimfuatilia kwa makini huyu kocha mtaelewa kwanini Borussia Dortmund wamempa kazi .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…