Thread maalumu ya mchezo wa Masumbwi (BOXING)

screpa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Posts
10,857
Reaction score
15,866
Ndondi ni mchezo uliotoa magwiji wengi walioheshimika duniani kama Muhammad Ally, Mike Tyson, Evander, Lewis, na wengine wengi. Kwa miaka kadhaa mchezo huu uliokuwa maarufu duniani ulionekana kupoteza mvuto baada ya majina makubwa kama Tyson kutoka kwenye 'prime' na kustaafu. Hii ilitokana pengine na kushindwa kupata wakali wengine katika uzito huo wa juu kwa kipindi kirefu na kupelekea 'Klitcho brothers' kudominate kwenye hiyo division pasipo kupata upinzani wa uhakika, hii ilisababisha wapenzi/wadau wa masumbwi kuelekeza macho yao kwenye uzito wa chini kwa maana ndio kulionekana kuna watu bora kuliko huko 'heavyweight', hapo ndipo yalipopatikana majina makubwa kama Mayweather, Pacquiao, Canelo, n.k. Habari njema kwa sasa ni kwamba kuna uwezekano wa heavyweight division 'division pendwa' kurudi kwenye ubora wake, kwa maana at least kuna majina kadhaa ambayo yanaweza kuandaa mapambano , majina kama Antony Joshua, Wilder, Tyson Fury, Whyte, Parker,n.k. Lengo la uzi huu ni kuwaunganisha wapenzi wa masumbwi ili kupeana updates ya mapambano hasa makubwa yanayofanyika sehemu mbalimbali ulimwenguni ikiwemo na Tanzania. Karibuni wadau!!!!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. ni mchezo ambao wewemchezaji ukitegea unakufa tofaouti na football
2. ni mchezo ambao mashabiki wanaupenda lakini hawawezi kuucheza
3.ni mchezo ambao hata kama umedundwa umelowa damu vip utapata nusu ya zawadi ya mshindi.
 
1. ni mchezo ambao wewemchezaji ukitegea unakufa tofaouti na football
2. ni mchezo ambao mashabiki wanaupenda lakini hawawezi kuucheza
3.ni mchezo ambao hata kama umedundwa umelowa damu vip utapata nusu ya zawadi ya mshindi.
Yap, kama mkataba unasema utapewa mil 10, hata ukidundwa hela yako inabakia ileile
 
Pambo la uzito wa juu lililopangwa kuwakutanisha bingwa wa Masumbwi duniani Antony Joshua 'AJ' na Jarrel Miller 'Big Baby' June1 limeahirishwa kutokana na Jarrel Miller kugundulika anatumia madawa ya kuongeza nguvu. Hata hivyo promoters wa pambano hilo hawako tayari kula hasara, wanalazimika kutafuta bondia mwingine atakayezichapa na AJ siku hiyohiyo, je atakuwa nani? Let's wait n' see....
 
Ni madawa yaliokatazwa, ingekuwa dawa za kuongeza nguvu angepelekwa mahakamani moja kwa moja
 
Jarrel Miller amefail second drug test, tutegemee ban ya mda mrefu hapa
 
Je Ortiz 'kingkong' kureplace pambano??
 
Kesho tar 20 April kuna pambano la kukata na shoka kati ya Crawford 'bingwa wa uzito wa welterweight' na muingereza anayerusha ngumi kwa speed ya light Amir Khan, upi utabiri wako hapa? Kwangu mimi natabiri Crawford kushinda kwa KO Round ya 9
 
Crawford vs Khan, hizi ndizo rekodi zao
 
Crawford has confidence
 
Pambano la Amir Khan na Crawford litapigwa asubuhi hii baada ya mapambano ya utangulizi
 
Stevenson vs Diaz, LIVE!!!
 
Pambano lenyewe ndo linaenda kuanza #CrawfordKhan
 
Pambano linaendelea Round ya pili
 
Crawford kashinda kwa TKO 6th Round
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…