screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,857
- 15,866
Ndondi ni mchezo uliotoa magwiji wengi walioheshimika duniani kama Muhammad Ally, Mike Tyson, Evander, Lewis, na wengine wengi. Kwa miaka kadhaa mchezo huu uliokuwa maarufu duniani ulionekana kupoteza mvuto baada ya majina makubwa kama Tyson kutoka kwenye 'prime' na kustaafu. Hii ilitokana pengine na kushindwa kupata wakali wengine katika uzito huo wa juu kwa kipindi kirefu na kupelekea 'Klitcho brothers' kudominate kwenye hiyo division pasipo kupata upinzani wa uhakika, hii ilisababisha wapenzi/wadau wa masumbwi kuelekeza macho yao kwenye uzito wa chini kwa maana ndio kulionekana kuna watu bora kuliko huko 'heavyweight', hapo ndipo yalipopatikana majina makubwa kama Mayweather, Pacquiao, Canelo, n.k. Habari njema kwa sasa ni kwamba kuna uwezekano wa heavyweight division 'division pendwa' kurudi kwenye ubora wake, kwa maana at least kuna majina kadhaa ambayo yanaweza kuandaa mapambano , majina kama Antony Joshua, Wilder, Tyson Fury, Whyte, Parker,n.k. Lengo la uzi huu ni kuwaunganisha wapenzi wa masumbwi ili kupeana updates ya mapambano hasa makubwa yanayofanyika sehemu mbalimbali ulimwenguni ikiwemo na Tanzania. Karibuni wadau!!!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app