THREAD ya ku-expose aina tofauti za utapeli unaofanyika ili tusaidiane kutoingia kingi kirahisi.

THREAD ya ku-expose aina tofauti za utapeli unaofanyika ili tusaidiane kutoingia kingi kirahisi.

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
Wauzaji feki wa sabuni za kuoshea choo:
Unakuta wame print kabisa na tshirt ya jina ya biashara yao. Wana target wale wanaonunua jumla. Ukifungua sabuni unakuta mimaji milaini mitupu.

Wanaojifanya Afisa wa TRA:
Unakuta mfanyabiashara anapigiwa simu na mtu anaejitambulisha kama mfanyakazi wa TRA katika wilaya uliopo. Anakuambia kuwa tunaona katika system utoaji wa risiti wako sio wa kuridhisha kabisa au anaweza kukuambia chochote cha kukuingiza mkingi then anakuambia umtoe hata 50k ili atulize makali ya ishu yako ili isifike juu ukapigwa faini.

Wanaojifanya afisa wa MKUKUTA:
Hii tusaidie wale wazee wetu maana wanapigwa sana. Unakuta tapeli anapata namba ya mzee ambae anaishi maisha duni then anamwambia tuna mpango wa kukusaidia ila kuna gharama zinahitajika za kujiunga na mpango huu.

Wale wa weka 10,000 upatiwe mkopo wa 100,000.
Vijana wengi wameitika hapa, haswa wale walioanza kushika simu za smartphone juzi juzi. Yeye anadhania kila kitu ni legit kwenye mtandao.

Wale wa kujifanya demu mkali mtandaoni ili wale nauli zenu:
Kuna akaunti nyingi huko mitandaoni ambazo zina picha ya demu mkali huku zikiwa na followers wengi lakini anaendesha ni jamaa yuko kwa shemeji yake kucha ajakata mwaka mzima na ameeka miguu juu ya sofa. huku akimuagiza juice beki tatu wa dada yake.

KARIBUNI KWA MBINU NYINGINE ZA KITAPELI..
 
Hawa wapo wengi, kuna gazeti moja nilishika kusoma nikakuta kila kurasa kuna tangazo la kujiunga na freemason au mganga kiboko ya wachawi katoa misukule saa sita mchana, hivi hii inaruhusiwa kisheria
Nashangaa mkuu, gazeti kabisa lina tangazo la kujiunga na freemason
 
Back
Top Bottom