Three things that will never change

chief1

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2015
Posts
1,418
Reaction score
1,449
Umuofia kwenyu!

Worth sharing;

Iwapo dunia hii isipogongwa na sayari ya nubiru na kuifutilia mbali, au sayari hii ya dunia isipo patwa na janga lolote la kuifanya isiwepo, kuna vitu VITATU TU ambavyo havitakuja kubadilika, watu,miti,majengo,bahari vyote vyaweza kubadilika,lakini hivi vitu VITATU havitobadilika mpaka siku ya kiama.

Tusome kidogo;

Genesis8:22

While the earth remaineth, seedtime and harvest, and cold and heat, and summer and winter, and day and night shall not cease (KJV).

Kuna vitu vitatu hapo:-

1. seedtime and harvest

2. seasons(summer and winter, heat and cold)

3. day and night

Nataka kuzungumzia zaidi hiyo ya kwanza(seedtime and harvest) maana hivyo vingine viwili vinaeleweka kwa urahisi.

Seedtime and harvest (mbegu-muda-mavuno):

Hapa kwa maana rahisi kabisa ni kwamba moja ya vitu ambavyo havitobadilika hapa duniani ni kwamba, unapopanda mbegu yeyote ile mahali popote ni lazima uipe muda ili uweze kuvuna , (hapa mbegu yako inaweza kuwa,idea,nguvu,kazi nk), jamani tusipopanda hatuwezi kuvuna hata siku moja, na tunapopanda ni lazima tuzipe muda hizo mbegu zetu ili tuweze kuvuna, huwezi ukapanda leo halafu utegemee kuvuna kesho(hata mchicha huchukua wiki mbili kutoka kupandwa mpaka kuvunwa), hapa ndipo mwanadamu anapokosea, au labda kwa sababu ya kukosa maarifa (hosea4:6) pata maarifa haya ili usiangamie ndugu yangu,kumbuka hii principle haitobadilika mpaka mwisho wa misingi ya ulimwengu.

Swala la muda wa mbegu kukua na kuzaa matunda ni la muhimu sana na linatofautiana kutokana na aina ya mbegu yenyewe, mbegu ya maembe au machungwa ni tofauti na mbegu ya mahindi au njegere, ni ukweli kwamba mbegu ya maembe inachukua muda mrefu mpaka kukua na kuzaa matunda, lakini matunda yake yana matokeo ya muda mrefu(endelevu),tofauti na mahindi unapata matunda kwa muda mfupi lakini matunda yake si endelevu:

kumbe sasa, matokeo makubwa na endelevu yanahitaji muda wa kutosha kuyafikia(hii haitobadilika),hata mimba ni lazima ipandwe kwanza halafu lazima ikae tumboni miezi 9 ndipo iweze kutoa matokeo kamili, ikitoka kabla ya muda wake maana yake imeharibika(abortion) na hapati matokeo yaliyotarajiwa, sasa wewe kijana mwenzangu mbona unataka kuvuna usipopanda? Mbona unataka kuvuna mahindi wakati ulipanda mchicha????utakufa,utakuwa aborted!

Unakuta kijana kaanzisha kampuni au wazo Fulani la biashara halafu anataka matokea makubwa baada ya muda mfupi,?how? haiwezekani !, matokeo makubwa yanahitaji mbegu inayochukua muda mrefu.

Wengi wanakata tamaa na kuyaacha mawazo yao yanakuwa aborted kwa sababu hawakuvumilia kufika muda wa kutoa matokeo, kuna watu wamefanya abortion mara nyingi sana maishani mwao, anaanza hiki anaona hakifai,anaanza kingine nacho hakifikishi mwisho, kaka/dada yangu mbona unaua mawazo hivyo?(an idea is a real thing). Kumbuka, seedtime and harvest will never change. usipovumilia muda wa mbegu yako kutoa matunda, utasubiri sana,changamoto zipo lakini ni lazima uvumilie na kupambana nazo mpaka mbegu yako izae matunda,

Lalamikia serikali sana, tukana sana, kama hujapanda hutovuna, na unapopanda usipoipa muda mbegu yako hutovuna!

SEEDTIME AND HARVEST WILL NEVER CHANGE!!

CEO!
 
Yayayayaaa Mpanzi alipanda mbegu... Zenye udongo mdogo zilinyauka... Thanks Chief 1
 
Nmeingiza kitu kichwani leo. Thanks mdau
 
Kweli kuna watu mnatupa nondo hatari. THANX MKUU
 
kwanza umekosea hamnaga sayari inayoitwa nubiru (ni nibiru na siyo nubiru kama ulivyoandika) hii nibiru ni orbit ambayo imaingiliana na orbit ya dunia ambayo sayari inayopatikana viumbe aina ya anunnaki (mi naamini hii ni myth kwa kuwa ina crash scientific laws about unirvese and space na hamna ki2 kama hicho kitakachokuja kutokea )
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…