Aha, nimesoma somewhere kwamba kumbe CREWS walikuwa-instructed to fly in total RADIO silency!!! Nafikili hili lilikuwa na tactical error kwa upande wao, wanawezaje kuruka kwa kupitia route yenye terrain ambayo hawako familiar nayo, huku waki-maintain RADIO silency hii ina maana wasingeweza kuwasiliana na the nearest Control Tower for HELP, au kupewa UPDATES kuhusu hali ya HEWA!! Wanasema plan za kufanikisha safari hii ziliandaliwa kwa muda wa miezi mitatu - sasa mahandalizi yalishindwaje kuwa na contigency plan just in case.
Oh yes, Kabaridi umenikumbusha kitu kinacho hitwa VENTURI effect. Jinsi nilivyo ona kwenye TV hali ya hewa ilikuwa mbaya sana, kulionikana kuna mist, mvua, baridi, upepo na altitude kama hile ya Mt. Kenya huwezi kokosa barafu - hatari katika urushaji wa Helicopter unatokea wakati main rotor inapo accumulate ice inasababisha madhala mawili-la kwanza ni kuongeza drag kwenye rotor blade, cha pili ambacho ni hatari zaidi ni kupungua kwa lift kutokana na mabadiliko katika aerodyanamic characteristics za main rotor yenyewe baada ya kuzungukwa na barafu, kumbuka main rotor ya chopper ina kazi mbili (i) Propeller (ii) Bawa i.e Wing, inaelezwa kabisa kwamba usihatarishe maisha yako kwa kurusha chopper/ndege kwenye icing conditions.
La mwisho, kumbe Gunship aina ya MI-24 zimekuwa design kuruka umbali wa mita 4500 kutoka usawa wa bahari(above sea level), wakati urefu wa Mt. Kenya ni mita 5199!! Swali ni je, marubani hili hawakulijuwa? Hapa tumelezwa kwamba chopper ya nne aina ya MI-17 ambayo ni ya kubeba troops iliweza ku-clear Mlima huo na kwenda kutua Somalia bila matatizo! Ukiangalia takwimu unakuta kumbe Chopper ya aina ya MI-17 ceiling ya urukaji wake juu ya usawa wa bahari ni mita 6000 yaani urukaji wake unahizidi MI-24 kwa mita karibu 1500, je katika urusha wa ndege hizo zenye specs tofauti marubani walishindwa kulizingatia hilo. Hapa natoa maoni yangu tu siyo kwamba nalahumu mtu au kikundi chochote.