Kwanza angalia huyo mtoto ana umri gani. Usijaribu kumkemea sana mtoto aliyechini ya miaka mitano kwa kukojoa kitandani, unamjengea woga maishani mwake na atakosa kujiamini. Kuna kittu inaitwa anal stage, tafadhari google utaelewa vitu vingi sana na utajiuliza mara mbili mbili kabla hujaamua kumhukumu myoto wako kwamba ni kikojozi. Na pia check kama huyo mtoto anatumia pampasi. Mara nyingi watoto wanaotumia pampasi huchelewa kuacha kujikojolea kwa sababu wamezoea kukojoa saa yoyote bila mkojo kuwaamsha. Ni tofauti sana na mtoto aliyekuzwa kwa nepi, maana huyo akikojoa mkojo humuwasha , na kama mama yake ni mtu msafi, atambadilisha haraka, na hivyo kumfanya mtoto ajijengee mazingira ya kuwa concious kabla hajakojoa. Kwa ufupi mtoto kuacha kukojoa ni process, na inategemea unamfundisahaje kutumia choo. Endapo unamkemea sana haisaidii zaidi ya kumtesa kisaikolojia na yeye kuanza kuchukia kitendo hicho. Mwisho mtoto anakuwa "defensive" na anajenga woga wa dhidi ya jamii inayomzidi umri, hivyo kuishia kuwa "yes" man huko ukubwani. Nakuomba tu ugoogle hilo neno "anal stage" utapata mwanga mkubwa sana!