Nilisoma humu namna ya kutibu maumivu ya kichwa kwa njia ya asili basi baada ya maumivu ya kichwa kunianza jana nikafuata ushauri wa tiba asilia kama nilivyosoma humu huku nikiamini nitapona.Ilipofika usiku kichwa kiliuma sana nikaamua kwenda msalani baada ya kwenda huko nikapoteza fahamu kuja kushtuka usiku najikuta niko msalani.Basi nikaamka nikaenda kulala ilifika asubuhi nikasema bora tu niende hospitalini baada ya vipimo kumbe ni malaria na ningechelewa hali ingekuwa mbaya zaidi.Kwakweli nawashauri dawa hizi za asili sio za kuziamini kwa asilimia miamoja.