Tiba mbadala imeniponza mwenzenu

Tiba mbadala imeniponza mwenzenu

SAYANSIKIMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2014
Posts
1,132
Reaction score
260
Nilisoma humu namna ya kutibu maumivu ya kichwa kwa njia ya asili basi baada ya maumivu ya kichwa kunianza jana nikafuata ushauri wa tiba asilia kama nilivyosoma humu huku nikiamini nitapona.Ilipofika usiku kichwa kiliuma sana nikaamua kwenda msalani baada ya kwenda huko nikapoteza fahamu kuja kushtuka usiku najikuta niko msalani.Basi nikaamka nikaenda kulala ilifika asubuhi nikasema bora tu niende hospitalini baada ya vipimo kumbe ni malaria na ningechelewa hali ingekuwa mbaya zaidi.Kwakweli nawashauri dawa hizi za asili sio za kuziamini kwa asilimia miamoja.
 
Hivi unaifahamu vizuri lugha ya Kiswahili?

Hebu soma tena kichwa cha habari halafu oanisha na ujumbe wako katika habari husika
 
yaani division 5 hazijaisha hata huku JF kunazo? mtu anashauriwa unafuata kama ndo mark scheme ? unatakiwa uongezee na zako
 
Nilisoma humu namna ya kutibu maumivu ya kichwa kwa njia ya asili basi baada ya maumivu ya kichwa kunianza jana nikafuata ushauri wa tiba asilia kama nilivyosoma humu huku nikiamini nitapona.Ilipofika usiku kichwa kiliuma sana nikaamua kwenda msalani baada ya kwenda huko nikapoteza fahamu kuja kushtuka usiku najikuta niko msalani.Basi nikaamka nikaenda kulala ilifika asubuhi nikasema bora tu niende hospitalini baada ya vipimo kumbe ni malaria na ningechelewa hali ingekuwa mbaya zaidi.Kwakweli nawashauri dawa hizi za asili sio za kuziamini kwa asilimia miamoja.

Wewe ndo mburula.Kwa nini ulitumia dawa ya kichwa badala ya kutibu malaria?! Ulitakiwa ukapime kwanza uhakikishe unaumwa nini.Hata ukitumia dawa za kisasa kutibu ugonjwa tofauti its the same thing.Acha upotoshaji
 
Maumivu ya kichwa ni dalili au kiashiria cha ugonjwa mwingine.. Sasa tiba mbadala ya nini? Hata matangazo ya Panadol na hedex yanasema maumivu yakizidi pata ushauri wa daktari
 
Ulilala chooni kwa muda gani mkuu manake dah!!

Kwakweli hata muda niliolala nilishindwa kuukadiria mimi nilishutukia nipo chini nimelala .ugonjwaa huu ukipanda kichwani ni mbaya sana.Fahamu zilipotea ghafla na namna nilivyo anguka hata sikumbuki mara ya kwanza natokewa na tukio hili.Kwa kweli kama mtu unaumwa kichwa usijaribu kutumia tiba mbadala ni hatari.
 
Back
Top Bottom