Umasikini na ujinga ni jambo baya sana. Watu wa tiba mbadala wanatapeli sana watu.
Ususani kwenye mambo wanayosema ni vipimo eti wana kipimo cha kupiga mwili mzima, na hicho kipimo mtu anashika kama pensel wanakutajia magonjwa kibao.
Pia wana kipimo kama kioo unaweka mkono wako kwenye kioo, wanasema eti linasoma mwili mzima.
Sasa hivi vipimo hata hospitali za serikali au hata hospitali kubwa kwa hapa ya tanzania hakuna.
Ninachoona ni umasikini na ujinga wa elimu ndomana watu wanaibiwa serikali iangalie watu wanatapeliwa sana.
Matapeli wapo kila tasnia ila huwezi kusema wote ni matapeli.
Hivyo vipimo sidhani kama vina shida yoyote isipokuwa shida inaweza kuwa;
1.Kukosa utaalamu wa kusoma na kutafsiri matokeo
2.Matokeo kutafsiriwa vizuri ila kukosa dawa sahihi ya kutibu ugonjwa husika
3.Kifaa husika kukosa matengenezo hivyo kushindwa kutoa matokeo sahihi.
Tulikuwa na house girl tulikaa nae badae akaolewa kijijini akapata mtoto,yule mtoto alisoma mpaka darasa la pili akaugua,akawa hawezi kusimama wala kukaa,ukimkalisha analala na akilala hana utulivu yaani anaweweseka hatulii,anatoka udenda,kula mpaka umlazimishe,kuongea hawezi zaidi ya kulia tu,wamezunguka huko Bugando,Hydom nk anaambiwa ubongo una shida,mara misuli anapewa dawa haponi na shule alishaacha,kuna daktari wa tiba
mbadala tulifahamiana nae(alimtibu maza) sasa yule binti alipomsimulia maza Kuhusu mtoto akaambiwa mlete nyumbani(mjini)yule dokta amuone,alipopimwa kwenye hicho kimashine(unavaa headphone fulani) ikaonyesha ubongo wake hauna shida isipokuwa mishipa ya fahamu(nerves) ndio zina shida na pia cells nyingi zimekufa.
Wakaambiwa atapona ila dawa zake ni kama 1.2M mpaka anapona,nayeye hakuamini kwanza aliona gharama kubwa pili akasema amezunguka hospitali kubwa kwahio akaona mtu mmoja tu na machine yake amtibu haiwezekani.Maza akamsihi(akimpa ushuhuda wa yeye kupona)wakakubaliana na Mme wake waanze tiba,ikabidi wauze mahindi ili walipe malipo ya awali mtoto aanze tiba wakati wanatafuta nyingine.
Ameanza tiba hapa home nikiwepo,wiki mbili za mwanzo mtoto akaanza kukaa,wakaenda kwao huku wakitumia dawa,baada ya miezi miwili walipokuja tena alikuwa tayari anatembea na kuongea vizuri,akapimwa tena na kupewa dawa za mwisho,wakati anaendelea kutumia tayari akarudi shule hata wakipiga simu katoto kanaongea vizuri tu,mpaka sasa hana shida yoyote,hata mimi mpaka leo huwa nastaajabu
Huyu nimemuona kwa macho sijasimuliwa,maana alikuwa nyumbani hapa kwa wiki 2 na aliporudi alinikuta,hata picha zake ninazo.
Pili hata kumjua huyu dokta kuna mama mtaani hapa figo zake zote zilifeli alikuwa Benjamin anafanyiwa dialysis,mama akachoka akaona anawafilisi watoto tu,akasema nipelekeni nyumbani nikafe,walipokutana na huyo dokta akapimwa na kuanza tiba,baada ya miezi minne akaanza kufanya usafi wa nyumba mwenyewe na shuguli zote,akawa kapona kabisa,hata watoto hawakuamini.(siku mama yangu ameenda kumuona alimkuta anafanya kazi mwenyewe ndio akamsimulia hali yake ilivyokuwa.
Kwahio tiba mbadala wapo tena vizuri mno hasa kwa magonjwa yasiyoambukiza yanatibiwa vizuri kuliko hata upande wa Pharmaceuticals.