1800, Pole..
Ningependa kuanza kwa kusema kuwa ni ugonjwa wa Pneumonia(Homa ya mapafu) na si "Nimonia".
Daktari, sasa hivi 'Nimonia' ni kiSwahili rasmi (official) cha 'Pneumonia', na si 'homa ya mapafu' wala 'kichomi' tena. Nimeshiriki katika mchakato wa kutengeneza IEC materials kwa ajili ya ujio wa chanjo mpya dhidi ya kuhara (rotavirus vaccine) na Nimonia (Pneumococcal vaccine) zitakazozinduliwa wiki ijayo, na kulikuwa na debate kubwa sana kuhusu jina gani linaeleweka kirahisi na jamii. Na katika utafiti uliofanyika, ilionekana wazazi na walezi wanajua Nimonia kuliko homa ya mapafu au kichomi...hivyo guidelines zote sasa ninaita Nimonia.
1800, Pole..
Ningependa kuanza kwa kusema kuwa ni ugonjwa wa Pneumonia(Homa ya mapafu) na si "Nimonia".
Pili, ningependa kusema tiba ya Homa ya mapafu ni dawa za Antibiotics, lakini dawa hizi hutegemea vijidudu(bacteria) waliosababisha Homa hii, Umri wa mgonjwa..nikiwa na maana Bacteria mbalimbali huweza kuleta tatizo hili katika umri tofauti(mf. wazee, watoto, watu wenye magonjwa ya upungufu wa kinga, na kwa baadhi ya magonjwa ya kurithi).Hivyo kwa kutegemeana na takwimu, vipimo alivyopimwa mwanao antibiotics husika hutolewa.
Asthma(Pumu), Kuna mengi yalikwisha ongelewa kuhusu hili katika thread za hapa JF Doctor, ingekuwa vizuri kupitia(ukijielimisha na kuongeza ufahamu kuhusu hili) lakini pamoja na hayo ningesema, Ugonjwa wa Pumu ni ugonjwa wa muda mrefu, hutibika(KUPUNGUZWA TATIZO), kutegemeana na number ya/za mashambulizi(attack) zinazotokea ikiwa ni kwa wiki/mwezi..Hivyo umwelezapo daktari, mara ngapi mtoto anashambuliwa("banwa na pumzi", anashindwa kupumua, n.k) huweza kukupa tiba inayofaa.
Ni vizuri kujua kuna baadhi ya vitu vinavyopelekea/vinavyochochea hali hii ya "kubanwa" (Asthmatic attacks) kutokea zikiwepo baridi, allergy n.k.
Allergy(pia kama tatizo la Asthma lilikwisha elezwa hapa), hata hivyo ni vizuri kuepuka allergens(vitu vinavyosababisha/chochea) tatizo mf. vumbi, marashi, baridi, manyoya ya wanyama, maua na baadhi ya mimea hasa ikianza kuchavua(kutoa pollen) n.k.
Hivyo basi ni muhimu, kuepuka mazingira hatarishi yanayoweza kusababisha attacks.
Mkuu 1800 Pole sana kwa huyo mtoto kuumwa na hayo maradhi. Dawa Ya Kifuwa Kwa Watoto Na Watuwazima.
Kwa Uwezo Wa Mwenyeezi Mungu Inshaallahu Atujaalie Shifaa Aamin
Chukuwa Asali Weka Kitunguu Maji Kikatekate Kichanganye Kwenye Asali Kiweke Masaa 12 Halafu Tumia Kiasi Kama Kipimo Cha Hospitali.
Inshaallahu atapona mtoto wako usikose kuleta feedback.
Pamoja na ushauri mzuri wa wadau hapo juu hasa Ashadii juu ya kumhifadhi kutokana na baridi, ushauri wa pili ni kufanya "allergy test". Hii itakusaidia kujua ni nini kunaleta hiyo Ashtma = Allergy reaction na kuviepuka, baada ya muda atakuwa ok. Pneumonia inatibika kwa hizo dawa za hospitali na "kumhifadhi"= Kuhakikisha hapatwi na ubaridi iwe mchana au usiku, hivyo hakikisha anatiwa haraka hiyo. Usisahau maombi kwa Mungu katika jina la Yesu yanaweza kufanya mambo makubwa kuliko tuyawazayo au tujuayo.
Madactory wengi hutoa sababu ya ugonjwa kwa kukisia.Mi mwanangu akiwa na miaka 3 alikua anakohoa sana.Nikaenda kwa mtaalamu wa kifua akasema ni pumu inamsumbua.Aliniandikia dawa mfuko wa Rambo ulijaa.Nilipofika home nikazisoma moja baada ya nyingine then nikazitundika.Nikaenda Dukani nikatafuta dawa ya kikohozi ya maji yenye mchanganyiko wa kupunguza mziho (BENYLIN ya watoto).Baada ya siku tatu akapona kabisa.Baadae nikagundua mtoto anakunywa sana maji ya baridi,then nikapiga marufuku.Kuhusu Nimonia,kuna dawa inaitwa Augment ya UK ni nzuri sana au Clavam
mkuu pole sana kwa kuuguza, ninachoweza kukusaidia mimi ni namba ya huyu mdingi ambaye anatengeneza dawa ya miti shamba ya pumu, kiukweli wengine niliowai kuwapa namba wanasema dawa yake imewasaida, dawa yake inarange kwenye 35000 mpaka 40000 kwa chupa, wewe mpigie maeelezo mengine atakupa yeye mwenyewe anaitwa mzee Pongwe 0715242033
Mkuu 1800 Asali iwe asali mbichi safi ya nyki kiwango chake fanya kiwe kama kikombe cha kahawa na kitunguumaji kiwe kimoja tu Kikatekate Kichanganye Kwenye Asali Kiweke Masaa 12 Halafu Tumia Kiasi Kama Kipimo Cha Hospitali. tumia kwa muda wa siku 3 kisha uje hapa utupe maendeleo ya Mwanao yanakwendaje? Give me feedback.Asante kwa ushauri juu ya dawa hii ya asili,ila labda unisaidie kitu,je asali ni kiwango gani na mchanganyiko wa kitungu uwe kwa kiwango gani!ahsante sana ndugu