Tiba ya Asthma,Nimonia kwa mtoto mdogo

aisee pole sana, mpeleke tu hospitali kwa specialist wa watoto, atapewa dawa zitamsaidia kwa hali hiyo, akishapona uendelee na za mitishamba, nami wanangu wana tatizo hilo ni wa miaka 1 na 3, ntasubiria feedback toka kwako kuhusu dawa za kina Mzizimkavu
 
Mi mwanangu amekohoa sana kuanzia miaka mitatu mpaka sita, sasa anaelekea miaka saba naona amepata nafuu, kamuone dr nsomokela pale amen opposite na palestina sinza anaweza kukusaidia, no.0754282332, na pia hiyo dawa ya benlin ya watoto ilimsaidia, hivyo vitunguu, asali nilitumia sana lakini haikusaidia, halafu kuhusu baridi mvalishe sweta lakini usimrundike manguo mengi akitokwa na jasho, ule unyevu unasababisha nimonioa




 

Asante kiongozi,dogo amesha onana na specialist na amepewa tiba na sasa yuko ok,ila dhumuni langu kuu ni kumpa tiba ya kienyeji ili kuangamiza kabisa lisije jirudia tena,na kwa sasa ndio nimeanza kumpa tiba za wadau walizoshauri hapa,nitaleta feedback wakuu
 

Asante kwa ushauri mkuu
 
Samahani kwa kuchelewa kujibu mzee wangu nilikuwa porini nafanya kazi
maelekezo ni
Tafuta mpapai dume chukua mizizi yake (hata mzizi mmoja tu unatosha)
kata vipande saba
Tafuta ufuta mweupe (nenda sokoni) ni kama kiasi cha robo kilo
Kaanga ufuta uwe mweusi
ipua na poza
chukua mizizi ya mpapai dume na changanya na ufuta uliokangwa na weka maji lita moja na nusu
chemsha hadi yabaki lita moja
ipua na uwe unampa kijiko kidogo kimoja kutwa mara tatu kwa muda wa siku saba mfululizo
waweza tengeneza mchanganyiko huu kila baada ya siku mbili ila kama unasehemu ya kuhifadhi dawa uliotengeneza vizuri haina shida kama hauna fanya kama nilivyokuelekeza kila baada ya siku mbili
Kwa mtu mkubwa ni kijiko kikubwa
Inshallah atapona na waambie wengine wenye matatizo kama haya
Haina masharti yeyote cha msingi ukianza dozi amalize usije ukaona anaanza kupona ukaacha na kama bado nenda siku kumi na nne
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…