Tiba ya babu wa Loliondo ya magonjwa sugu ni batili.

Tiba ya babu wa Loliondo ya magonjwa sugu ni batili.

mayoscissors

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2009
Posts
975
Reaction score
478
Wana jamii forum leo nimekutana na mgonjwa mwenye kisukari ambaye alipata dawa ya mchungaji wa loliondo na hali yake ilikuwa mbaya sukari ilikuwa juu sana na ilibidi nimshauri aanze insuli ambayo alikuwa nayo hata alipoanza safari kwenda kwa babu,Kwa mtazamo wangu eweni makini njia za mkato zina mjuto baadae
 
Wajamani,kwa babu NI IMANI!!!.... OTHERWISE USIPOTEZE MUDA WAKO KWENDA HUKO.
 
We kijana langei, nakupa ushauri wa bure, futa hii thread, maana inakudhalilisha na unaonekana huna akili.
Nduguyo au nyie mliompeleka hamna imani, na mlikuwa mnamjaribu babu.
Mtu aliekuwa na sukari, na akatibiwa na babu akiona unachoandika hapa atakudharau sana mkikutana physically.
Unatakiwa ufanye uchunguzi japo wa sample ya watu wa5 ndio ufanye fluke iliyobobea kama hii.
Usifanye mzaha na imani bana, na wala usiwatie watu majaribuni.
All in all POLE.
 
Wana jamii forum leo nimekutana na mgonjwa mwenye kisukari ambaye alipata dawa ya mchungaji wa loliondo na hali yake ilikuwa mbaya sukari ilikuwa juu sana na ilibidi nimshauri aanze insuli ambayo alikuwa nayo hata alipoanza safari kwenda kwa babu,Kwa mtazamo wangu eweni makini njia za mkato zina mjuto baadae

Huyo lazima alichakachua, maana yake, 1 hakuwa na imani alienda kujaribu tu,2 alipita watu wengine kwenye foleni.
 
Huyo lazima alichakachua, maana yake, 1 hakuwa na imani alienda kujaribu tu,2 alipita watu wengine kwenye foleni.

As a medical student it is always facinating wen I see discussions kuhusu "Babu", lakini kuna mkanganyiko mmoja ambao unajitokeza hapa,wote kwa ujumla tunataka mafanikio as far as health is concerned. Huduma anayoitoa babu ina malengo yale yale kama kwenye kituo chochote cha afya na hivyo wafanyakazi wote wa afya hawana budi kuiombea mafanikio huduma hiyo.
 
Mie Kama mwanasayansi. "tiba" ya babu Kama mnavyoiita ni uzushi mtupu. Hakuna hata mtu mmoja aliyekuwa Anaumwa kweli amepona. Namsupport aliyeanzisha thread, Kama kweli unaumwa na umeacha dawa utakuja kujuta!
Nyie mnaokuja na hoja zenu za Imani Mna matatizo ya kisaikolojia Kama babu yenu wa loliondo -sorry kuwapa ukweli wenu.
Bilious mtu anachangia hapa nadhani ameelimika (kidogo) lakini ukweli ni kwamba hamjaelimika na bado mnaishi Kama babu zetu miaka ya 1900s inasikitisha sana na Ndio maana Tanzania hatutaendele kamwe! Ndio maana na viongozi wenu wanashabiki mambo ya loliondo. Sijui mkoje???!
 
Nampongeza aliyeanzisha hii thread. As critical thinkers we need to look at everything critically. Lakini cha ajabu sana hapa JF mtu akigusa mambo ya babu watu wanampigia kelele anyamaze. Pamoja na claim nyingi za watu kupona hakuna aliyethibitishwa kitaalamu, ingawa kuna watu wengi sana waliopata hicho kikombe na sasa wamekufa. Inasikitisha, lakini huo ndio ukweli wenyewe. Hii tiba ni ganga wa kienyeji na wanaosema ni imani naomba niwaulize, ni imani katika nini? kikombe? au babu? au mgarika? au loliondo?
 
Wana jamii forum leo nimekutana na mgonjwa mwenye kisukari ambaye alipata dawa ya mchungaji wa loliondo na hali yake ilikuwa mbaya sukari ilikuwa juu sana na ilibidi nimshauri aanze insuli ambayo alikuwa nayo hata alipoanza safari kwenda kwa babu,Kwa mtazamo wangu eweni makini njia za mkato zina mjuto baadae

Imani(kwa wanaoamini) kama ni haba huwezi pona,usimjaribu babu
 
tiba ya babu ni kizungumkuti, sijabahatika kukutana wala kusikia aliyepona kiukweli bali ambao wameenda lakini wamerudi vile vile au hali imekuwa mbaya zaidi. Kiukweli hiyo imani haieleweki ni ya nini, babu, kikombe au Mwenyezi Mungu? Tunathibitishaje kwamba babu ameoteshwa na Mungu na sio mizimu ya kinyakyusa? Anyway, wenye imani zao waendelee kusongamana huko loliondo, lakini wengi wataishia majuto.
 
Babu hana lolote isipokuwa ni kutumiwa na viongozi au kundi fulani la watu kuwapumbaza watanzania kuwa dawa hiyo imetoka kwa Mungu.

Hakuna kitukibaya kama mtu kuharibikiwa kisaikolojia kwani anaweza akahisi kupona kumbe hajapona.Kuthitisha kupona mbona hawaendi kupima hospitali? na kwanini babu kila siku anaongeza siku za kupona/ kwani alisema siku saba mwisho mara siku kumi na nne mara miezi mitatu.

Kinachotakiwa watanzania tufunguke macho.
 
Nilivyosikia, sukari wengi, sio wote ila wengi imegonga mwamba lakini magonjwa mengine watu wanasema wamepona. Ni mapema pia kutoa conclusion.
 
Wana jamii forum leo nimekutana na mgonjwa mwenye kisukari ambaye alipata dawa ya mchungaji wa loliondo na hali yake ilikuwa mbaya sukari ilikuwa juu sana na ilibidi nimshauri aanze insuli ambayo alikuwa nayo hata alipoanza safari kwenda kwa babu,Kwa mtazamo wangu eweni makini njia za mkato zina mjuto baadae

Acha kudanganya umma. Hata dawa za kizungu kama za malaria kuna baadhi zinawaponya na baadhi haziwaponyi. Sasa kwa nini ya Babu wa Loliondo iwe nongwa. Tusipende ku-geralize mambo hivyo!
 
hivi wew ulieandika hii thread umeenda kupta kikombe au kujamaa au rafiki au ndugu yko yoyote ambaye amepata kikombe akawa amegonga mwamba? Na kinacho takiwa sio kusikia inabd 2cbtishiwe kutoka kwa dr? Kama sikosei mwananchi ili mtoa mtu aliyepewa kikombe akapona na je yeye ni muongo pamoja na gazeti pia...maana hujatoa ushuhuda wowte so stop shout..
 
mwaka ukiisha suluhu haijapatikana samunge itabidi babu aende uhamishoni lasi hivyo atakipata cha moto kudanganya dunia
 
Aliyepona atujuze humu moja kwa moja badala ya kumtetea Babu bila Data.
 
Mimi ninaye shangazi yangu ambaye alikuwa anasumbuliwa sana na kisukari. Vyakula vingi aliacha kula lakini hivi ninavyoandika amepona kabisa. Anakula vyakula vya wanga kama kawaida na sugar ipo normal. Jamani kama kuna mtu hajapona basi asigeneralize. Wapo wengi tu wamepona na kurejea katika maisha yao ya zamani.
 
Mie Kama mwanasayansi. "tiba" ya babu Kama mnavyoiita ni uzushi mtupu. Hakuna hata mtu mmoja aliyekuwa Anaumwa kweli amepona. Namsupport aliyeanzisha thread, Kama kweli unaumwa na umeacha dawa utakuja kujuta!
Nyie mnaokuja na hoja zenu za Imani Mna matatizo ya kisaikolojia Kama babu yenu wa loliondo -sorry kuwapa ukweli wenu.
Bilious mtu anachangia hapa nadhani ameelimika (kidogo) lakini ukweli ni kwamba hamjaelimika na bado mnaishi Kama babu zetu miaka ya 1900s inasikitisha sana na Ndio maana Tanzania hatutaendele kamwe! Ndio maana na viongozi wenu wanashabiki mambo ya loliondo. Sijui mkoje???!

Hhaaaa Haaaaaa,
ndio tunaishi kisen.ge kama walivyoishi babu zetu (wasen.ge) enzi za majimaji! Risasi zilibadilika kuwa maji! lmao
 
Back
Top Bottom