Tiba ya babu wa Loliondo ya magonjwa sugu ni batili.

Tiba ya babu wa Loliondo ya magonjwa sugu ni batili.

dah, kwa kweli habari ya Loliondo ni kama kizungumkuti! Tusubiri watu wa NIMR wanaofanya study watupe majibu! Nina jamaa yangu daktari ambaye anahudumia wagonjwa wawili critical ambao walipita kwa babu na kupata kikombe. Ni wagonjwa na kisukari, pressure na mwengine anaishi na Virusi vya ukimwi na kisukari. HAWAJAPONA despite ya kupata kikombe!
Kuhusu suala la malaria kutibiwa na baadhi ya dawa kuwa hazitibu,kisayansi inajulikana kama drug resistance, na inatokea kwa dawa ambazo zimekuwa zikitumika kwa muda mrefu na jamii fulani, je vp kuhusu hii mpya ya babu!
Tuache ushabiki when it comes to reality na maisha ya watu!
 
Nashukuru kwa mawazo yenu na hoja zenu,wagonjwa wengi wa sukari wamekuwa wanakuja na hali wanaita kitaalam diadetic ketoacidosis na wengi wamepoteza maisha,naomba mkumbuke dawa zingine zilizowahi kupata umashuhuri kama ngoka eleven,wengi waliishia kupata renal failure.
Mimi natoka jamii inayotumia dawa za asili na dawa hizi zinatibu vizuri tu tena magonjwa maalum na wala si mafungu!
Sijui tutaficha wapi nyuso zetu pale ukweli utakapojulikana
all the best wana jf
 
kwakweli mimi nina mtu wangu wa karibu sana na ana kisukari.Niliposikia habari ya babu wa Loliondo nikafarijika sana, lakini sikuweza kumpeleka kwa haraka mpaka nifanye utafiti juu ya ufanisi wa tiba hiyo ya kienyeji.Katika pekua pekua yangu nimekutana na mambo ya ajabu sana haifai hata kusimulia.Lakini nitasema machache yanayosimulika na kwa faida ya umma.
1: Siku moja katika zahanati ya Dr. Abbas walikuja wagonjwa sita wa kisukari ambao hapo mwanzo walikuwa wanaattend hapo lakini walisitisha baada kupata kikombe na kuahidiwa kupona baada ya wiki moja. Basi siku hiyo ya tarehe 18 mwezi March waliletwa na hali mbaya sana baada ya kukaa wiki nzima bila kutumia dawa zao. Ikabidi wengine tusubiri wahudumiwe wao kwanza.
2: Kazini kwetu kuna mtu alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu lakini alikuwa na afya yake nzuri tu kwakua alikuwa anatumia dawa.hata hivyo baada ya kupata kikombe tu aliishi wiki mbili kafa na tumemzika.
3: Kuna mwalimu wa shule ya msingi huko Tabata alimpeleka mwanae.......... Lakini kilichompata jana hapo shuleni nadhani nitapata mtu wa kuthibitisha humuhumu jamvini.
4:Nilikuwa nasimulia kisa cha kwa Dr.Abbas pale Namanga kwa muuza magazeti, akatokea jamaa alikuja kununua nyama pale na akatuambia yeye mwenyewe ni mgonjwa wa kisukari na amekwenda kwa Babu lakini hakupona.
:. Cha muhimu hapa sijabahatika kukutana ana aliyepona kwa hakika. Na kuhusu kupona kwa imani, sawa waganga wote duniani usipopona hukupa sababu kama hizo za kushindwa masharti, imani na mengine mengi.
Labda tusubiri tunaweza kuprove otherwise.
 
Sijui hata pa kuiweka hiyo tiba ya babu kama inafaa au la! Nawafahamu watu 6 walioenda huko mmoja ana stroke yuko vilevile,wa5 wa sukari kati yao wa3 wanaendelea vizuri m1 tulishazika na mwingine tunasafirisha maiti yake leo.
 
Nakupongeza

Hakuna hata mmoja anayeweza kuthubutu kutamka kapona, hasa HIV

Watu wanakufa kwelikweli, labda ni mkakati wa serikali kuundoa ukimwi kwa kuwarubuni wagonjwa wapate kikombe kisha wafe kwa imani.

Kama kweli ingekuwa ni imani, basi babu angekwnda Ocean Road kuponya wagonjwa wa kansa, mimi ningelipa hizo 500 kwa wagonjwa wote waliolazwa pale na nauli yake.
Nampongeza aliyeanzisha hii thread. As critical thinkers we need to look at everything critically. Lakini cha ajabu sana hapa JF mtu akigusa mambo ya babu watu wanampigia kelele anyamaze. Pamoja na claim nyingi za watu kupona hakuna aliyethibitishwa kitaalamu, ingawa kuna watu wengi sana waliopata hicho kikombe na sasa wamekufa. Inasikitisha, lakini huo ndio ukweli wenyewe. Hii tiba ni ganga wa kienyeji na wanaosema ni imani naomba niwaulize, ni imani katika nini? kikombe? au babu? au mgarika? au loliondo?
 
mbona nilipost hapa jana kuhusu matukio ya watu mbalimbali walioenda kupata kikombe lakini leo siioni? au kuna uchakachuaji wa ushuhuda?
 
Au ni mkakati wa sirikali na chama cha magamba tusahau dowans?
 
Siku hz nmeacha kuisemea tiba ya babu. Sijawah kushuhudia m2 aliyepona. Nimewah kushuhudia wa2 watano wamekufa baada ya kikombe. Sielewi, elewi. Tusubiri tuone.
 
Tiba ya babu wa Loliondo ya magonjwa sugu ni batili.
Hiyo tiba ya hospitali kama si batili kwa nini aliiacha akaenda kwa babu? Je, akiendelea na matibabu ya hospitali bila kupona, utarudi humu tena kuweka thread kwamba "Tiba ya hospitali ni batili"?
 
Aliyepona atujuze humu moja kwa moja badala ya kumtetea Babu bila Data.
Mbona Augustine Lyatonga Mrema alisema amepona. Ilikuwa live TBC kwenye kipindi cha usiku wa habari tarehe 15/3/2011
 
Back
Top Bottom