ZOPPA
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 2,729
- 2,891
Mwalimu wa saikolojia aliingia darasani na bilauri ya maji. Baada ya kusabahiana na wanafunzi wake, aliinua juu bilauri ya maji na kuwauliza: "Kwa kutazama bilauri hii, pamoja na maji ndani yake, nani anaweza kunitajia uzito wake?"
Hakuna aliyeweza kujua uzito wa bilauri kwa kuipima kwa macho. Kuona hivyo, mwalimu alimwita mwanafunzi mmoja mbele ya darasa, na kumtaka ainyanyua bilauri ile juu kabisa kisha atoe jibu. Baada ya kunyanyua tu, mwanafunzi alisema: "Ina kama uzito wa nusu kilo."
Pamoja na kutoa jibu lake, mwalimu alimtaka mwanafunzi aendelee kuinyanyua bilauri vilevile. Haraka mwalimu akaenda mezani na kuanza kuperuzi vitabu vyake kwa takribani dakika tano. Aliporudi, akamuuliza tena mwanafunzi wake: "Ulisema ina uzito gani?"
"Ina kama kilo moja hivi," mwanafunzi alijibu. Safari hii akibadilisha jibu. Mwanzo alisema ina uzito wa nusu kilo.
Mwalimu akarudi tena mezani pake na kuendelea kuperuzi vitabu vyake kwa dakika kama zile za wali. Kisha akarejea mpaka pale aliposimama mwanafunzi wake na kumuuliza: "Sasa tuendelee na somo; umesema ina uzito gani vile?"
Mwanafunzi akajibu, "Naona kama ina uzito wa kilo mbili."
Kadiri muda ukivyokuwa unyoyoma, mkono ukaanza kumtetemeka mwanafunzi. Mara nguvu zikaanza kumwisha - mkono ukawa kama unataka kupooza vile, ndipo mwalimu akamuwahi kuichukua bilauri kabla hajaidondosha na kuivunja.
Mwalimu alipomruhusu mwanafunzi akaketi, akawaelekea wanafunzi wake na kusema: "Nadhani nyote mmeona, mwanzo mwenzetu alipoinyanyua bilauri, aliiona ya kawaida tu akasema ina uzito wa nusu kilo, lakini baada ya kuinyanyua kwa muda mrefu akaanza kuchoka na kusema ina uzito wa kilo moja, na alipoendelea kuinyanyua zaidi uzito kumzidia, akaanza kuhisi mchoko na maumivu, mkono ukaanza kupooza - mara akasema ina uzito wa kilo mbili. Kimsingi, bilauri haikuwa ikiongezeka uzito, bali kwa kadiri alivyoendelea kuinyanyua juu, ndivyo mikono ilivyozidi kuchoka kwa kuelemewa na uzito kiasi cha kumfanya aone bilauri ikiongezeka uzito. Mnajua maana ya somo hili?"
Darasa zima likapiga kimya. Mwalimu akaendea, "Msongo wa mawazo, huzuni na simanzi maishani mwa mwanaadamu ni sawa na hii bilauri ya maji. Unapofikwa na huzuni au msongo, mwanzo raha na amani hutoweka kiasi. Sasa kama utazitua chini huzuni na msongo, mambo utayaona mepesi. Lakini endapo utaruhusu kichwa chako kiendelee kubeba huzuni na simanzi hizo kwa muda mrefu, mara vitaanza kukuzidia uzito na mwisho utaanza kupooza mwili na akili - hatimaye utaangamia kabisa. Matatizo yakikufika, usiyabebe muda mrefu kwa kuyafikiria mno - yatue chini kwa kujifariji na kufurahi pamoja na familia au marafiki - kamwe machungu yake hayatokuangusha."