Kwa ufahamu mdogo nilio nao, leukemia (sina uhakika na spelling) haina tiba. Ngoja waje wataalam watusaidie hapa.
Ndugu, wana jf naomba kwa wale wenye uelewa wa tiba ya saratani ya damu, maana kaka yangu amepima amebainika kuwa nayo, na amelazwa hoptali ya rufaa ya Bugando, chanzo chako inawezekana ni kutoka mgodi wa north mara, maana alifanya kazi eneo la plant kwa muda wa mwaka mmoja, ameandikiwa dawa aina ya chlorambucil tabs 50mg po oD 3/52, tumejitahidi kutafuta kwa Mwanza bila mafanikio, naomba msaada wenu wa mawazo hata tiba kama ikipatikana.il Vilevile msaada wa sheria.
Nawasilisha.
kuna jamaa alitibiwa ocean road akapona, wasiliana na ocean road cancer institute kwa maelezo zaidi.
Mkuu Nonda hilo nalo ni neno!!! Ikiwa kuwa Baba Wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere hakuweza kutibiwa Tanzania kwa hayo Maradhi ya Kansa ya Damu basi hakuna Dawa za kutibu hayo Maradhi ya Kansa ya Damu (Leukemia) hapo Tanzania yetu labda nje ya nchi .Kwa nini walimpeleka Mwalimu UK kwa matibabu?
Kwa nini walimpeleka Mwalimu UK kwa matibabu?
naomba kujua tiba ya kansa ya kitaalamu au tiba mbadala tafadhalini.
Huyu ndugu yangu ana kansa ya anal na bladder, tumeshaonana na madaktari wanasema inabidi apasuliwa ili kupambana na shida hii.