Dr. Zaganza
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 1,814
- 2,738
Kifafa ni ugonjwa sugu wa neva unaosababishwa na mabadiliko ya ghafla ya mfumo wa umeme wa ubongo. Hali hii huleta mshituko na kusababisha mtetemeko (degedege), kukakamaa kwa mwili, na kupoteza fahamu
Dalili za Kifafa
Dalili hutegemea eneo la ubongo lililoathiriwa, lakini mara nyingi hujumuisha:
- Kuanguka ghafla chini na kutetemeka mwili mzima.
- Ugumu wa misuli (mwili kukakamaa).
- Kutokwa na povu mdomoni, kuuma ulimi, au kukojoa bila kujitambua.
- Kupoteza fahamu au kutazama angani kwa muda mfupi bila kujitambua
2.Kifafa kinachotokana na Uvimbe katika ubongo Kumbuka fuvu la kichwa halikui.Hivyo ubongo ukipata uvimbe,unalibana fuvu na kuongeza presha ya umeme na kuleta shoti,kila ikipiga shoti ,mgonjwa wa kifafa anaanguka. Vimbe katika ubongo zikipimwa na MRI hugawanywa sehemu 2.Vimbe ya kawaida na vimbe ya kansa. Tiba ya vimbe ya kawaida ni mimea ya kuondoa uvimbe wa ubongo kama mshinda na muosha fedha (wahaya wanaita umutwango na umuhuwe ).Tiba ya vimbe ya kansa hutibiwa kama kansa zingine ili kumaliza kifafa
3.Kifafa kinachotokana na minyoo sugu Minyoo kama Taenia solium ilioyoko kwa nguruwe,hukimbilia kwa ubongo ikiwa bado midogo.Ukila na yenyewe inakula ,na kukua.Ikifika mwisho wa nafasi iliyopo,kila ikijinyoosha kukua ,ndipo mgonjwa wa kifafa anaanguka.Tiba ya kifafa cha minyoo ni kuitibu minyoo kwa mimea kama Kindukuli na Mjaafari.
4.Kifafa kitokanacho na kushuka kinga za mwili Kama kinga zako zitashuka kwa sababu yoyote ile iwe HIV au magonjwa mbali mbali kama TB n.k , huleta kifafa.Kinga ya mwili (Auto Antibodies) huwezesha viungo kumudu kupokea umeme wa ubongo .
Endapo kinga zikashuka, hushindwa kumudu na kuonekana kama umeme ni mkubwa , kila kiwango kinapokusanyika na kuzidi kiwango fulani, mgonjwa huanguka. Tiba ni kupandisha kinga kwa mimea kama imsokonoi, mkandandogowe na gotukola.
Pia soma: Ufahamu Ugonjwa wa Kifafa na namna bora ya Kuishi na Wagonjwa wa kifafa