Tiba ya macho ya majani yanayoota pembezoni mwa mto

Village in

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2026
Posts
311
Reaction score
626
Kama kichwa cha habari hapo juu. Kuna rafikiangu kwa sasa ni marehemu alikuwa anasaidia yoyote mwenye tatizo la macho,hasa ile hali ya mtoto wa jicho au hata jicho linaloanza kuwa na uoni hafifu au kuwa kama na ukungu hivi.

Huyu jamaa yangu marehemu alikuwa anachuma majani fulani mabichi pembezoni mwa mto anayafikicha mkononi anakukamulia maji ya hayo majani kwenye macho. Yalikuwa yanauma sana akikukamulia yale maji Ila baada ya dakika 3 mpaka 5 hapo yanapoa,jicho linakuwa limesafishika jeuoe vizuri sana.

Bahati mbaya sana wote hatukuizingatia hiyo dawa.

SWALI LANGU KWENU KAMA KUNA MTU YOYOTE MWENYE KUYAJUA HAYO MAJANI NAOMBA MSAADA TAFADHALI. KUNA DOGO ANATEKETEA TUMUOKOE KWA HIYO TIBA.

Marehemu enzi za kukua kwake amekulia maeneo ya kamsamba,chunya (kama kuna watu humu waliokulia huko miaka ya kuanzia 80,90 hivyo)

NB;-NIKIYAONA NAWEZA KUYAKUMBUKA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…