Tiba ya maradhi ya katiba

Tiba ya maradhi ya katiba

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
"...Nina maradhi gani na katiba..?" Alilalama aliyepata maradhi...! Na nadhani maradhi yake ni haya

Alikuwa makamu mwenyekiti wake katika hilo bunge la katiba iliyoleta maradhi. Kwa ushirikiano wao wakaondoa maoni ya wananchi yaliyokusanywa na tume iliyoongozwa na Jaji Warioba. JK akaponda na hata kumponda mwenyekiti wake. Kijana mdogo kabisa Bashite akamkata ngwara na kuzawadiwa cheo cha ukuu wa wilaya Kinondoni. Wakaja na maoni ya chama fulani badala ya yale maoni ya wananchi. Othman Masoud Othman Sharrif akaadhibiwa kwa kuporwa cheo kwakuwa tu na mtazamo tofauti na chama fulani
Mpaka hapo lazima upate maradhi...Tena makubwa tuu...!!!

Sasa ni ipi tiba ya maradhi kama hayo?

  • Kwanza ni toba!
  • Pili ni katiba mpya yenye maoni ya wananchi wote, bila kujali chama fulani
  • Humo iwemo tume huru, wagombea huru, Zanzibar huru, Tanganyika huru nknk

Haya ni maoni yangu na nitaheshimu yeyote mwenye maoni tofauti na haya pasipo kubeza au kudharau au kukejeli..Heshima kwanza kwa utu wa mtu hata kama ana maoni tofauti au mtazamo tofauti.

Nawasalimu katika jina la Jamhuri...

Credit kwako Gwappo Mwakatobe
 
Mgosi malizia kabisa hapo chini! Asipofanya toba kwa kuurejesha upya ule mchakato wa Katiba kwa kujenga usawa kwa wajumbe wa makundi mbalimbali, badala ya kujaza wanasiasa! Basi na yeye ajiandae kwa KARMA!

Akilala, akiamka, akiswali, nk awe ana uota/kuukumbuka tu huo mchakato. Ubinafsi inawatesa sana CCM! Kiasi cha kujiona wana haki zaidi ya wengine kuitawala Tanzania, jambo ambalo si sahihi hata kidogo.
 
KARMA...[emoji848][emoji848][emoji848][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
 
IMG-20141102-WA0010.jpg
 
"...Nina maradhi gani na katiba..?" Alilalama aliyepata maradhi...! Na nadhani maradhi yake ni haya

Alikuwa makamu mwenyekiti wake katika hilo bunge la katiba iliyoleta maradhi. Kwa ushirikiano wao wakaondoa maoni ya wananchi yaliyokusanywa na tume iliyoongozwa na Jaji Warioba. JK akaponda na hata kumponda mwenyekiti wake. Kijana mdogo kabisa Bashite akamkata ngwara na kuzawadiwa cheo cha ukuu wa wilaya Kinondoni. Wakaja na maoni ya chama fulani badala ya yale maoni ya wananchi. Othman Masoud Othman Sharrif akaadhibiwa kwa kuporwa cheo kwakuwa tu na mtazamo tofauti na chama fulani
Mpaka hapo lazima upate maradhi...Tena makubwa tuu...!!!

Sasa ni ipi tiba ya maradhi kama hayo?

  • Kwanza ni toba!
  • Pili ni katiba mpya yenye maoni ya wananchi wote, bila kujali chama fulani
  • Humo iwemo tume huru, wagombea huru, Zanzibar huru, Tanganyika huru nknk

Haya ni maoni yangu na nitaheshimu yeyote mwenye maoni tofauti na haya pasipo kubeza au kudharau au kukejeli..Heshima kwanza kwa utu wa mtu hata kama ana maoni tofauti au mtazamo tofauti.

Nawasalimu katika jina la Jamhuri...

Credit kwako Gwappo Mwakatobe
Tiba ya katiba ni SSH akishindwa tusubiri mitume.
 
Ameonesha mwanzo mzuri

Back
Top Bottom