Tony Laurent
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 5,606
- 7,032
Naomba ushauri kwenu wataalamu wa masuala ya tiba. Nina ndugu yangu mwanamke ambaye amekuwa na matatizo ya kuumwa na miguu (feet) kwa muda mrefu sasa. Tatizo hili lilianza mara baada ya kujifungua miaka 11 iliyopita. Huwa anasema maumivu huwa makali zaidi anapokuwa ametembea kwa muda mrefu au kunapokuwa na baridi.Anasema kuwa wakati mwingine maumivu yake huwa kama ya kuungua na moto. Amejaribu kutafuta tiba sehemu mbalimbali, ikiwemo Hospitali ya taifa ya Muhimbili; lakini tatizo bado linaendelea. Huwa anapata nafuu ya muda tu.
Kwa yeyote anayefahamu tiba ya tatizo hili au hata kumfahamu mtaalamu wa tatizo hili tafadhali naomba anifahamishe ili mama huyu aweze kupata tiba ya kudumu.
Kwa yeyote anayefahamu tiba ya tatizo hili au hata kumfahamu mtaalamu wa tatizo hili tafadhali naomba anifahamishe ili mama huyu aweze kupata tiba ya kudumu.