Tiba ya tezi dume bila upasuaji inawezekana?

Tiba ya tezi dume bila upasuaji inawezekana?

LIFE HELP

Senior Member
Joined
Nov 29, 2012
Posts
149
Reaction score
71
Wakuu naomba kuelewa kwa yeyote anayejua au kushudia matibabu ya Tezi dume bila upasuaji na mgongwa kupona kabisa na hayo matibabu yanapatikana wapi?

Nitafurahi zaidi kupata taarifa za matibabu ya kisayansi kwa maana ya yanaweza kuwa wanatumia aidha dawa za asili au dawa mbadala au dawa za hospitali lakini matokeo yake yamethibitishwa kisayansi.

Natanguliza shukurani
 
Babu yetu aliumwa tezi dume sasa kutokana na umri daktari akashauri asifanyiwe upasuaji, tukampata mganga toka Tanga tukamleta Moro kumtibia babu. Baada ya mwezi tukampeleka kupima tezi dume haikuonekana na mpaka anakufa hakuwa na tatizo hilo tena, alikufa kwa uzee tu.

Kwa hiyo me nina uhakika matibabu ya tezi dume ya asili yapo na mtu anapona kabisa.
 
Babu yetu aliumwa tezi dume sasa kutokana na umri daktari akashauri asifanyiwe upasuaji, tukampata mganga toka Tanga tukamleta Moro kumtibia babu...
Hongereni kwa kufanikisha hili. Huyu mtalaam anapatikana Tanga sehemu gani
 
Dawa zipo na utapona kabisa bila hata ya kuhitaji upasuaji
Fungua PM yako mkuu kama kweli una hii dawa. Utasaidia wengi maana operesheni kama aliyofanya JK ni very risky kwa sababu kakosa kadogo tu mtambo mzima wa nyuklia unaweza usifanye kazi permanently not to mention incontinence na matatizo mengine kibao.
 
Matunda ni tiba hasa hasa machungwa mengi - citric acid kwenye machungwa ni nzuri sana kutibu / kupunguza makali ya tezi.

Pia, kuna kukamuliwa 🏃🏃🏃🏃
 
Tiba ya tezi dume hutegemea sana sababu ya tatizo hilo. Katika baadhi ya hali, kama vile kama kuna dalili za awali au dalili za wastani za tezi dume, daktari anaweza kupendekeza matibabu ambayo hayahitaji upasuaji. Baadhi ya matibabu haya ni pamoja na:

1. Dawa: Daktari anaweza kukuagiza dawa ambazo zinaweza kusaidia kupunguza uvimbe wa tezi dume na kupunguza dalili zako.

2. Upasuaji mdogo: Daktari anaweza kufanya upasuaji mdogo, kama vile Transurethral microwave thermotherapy (TUMT) au Transurethral needle ablation (TUNA), ambayo ni njia ambazo hazihitaji kufungua tumbo lako.

3. Tiba ya laser: Njia hii hutumia laser kwa ajili ya kuteketeza sehemu ya tezi dume inayosababisha dalili.

Ni muhimu kufuata maelekezo ya daktari kuhusu matibabu yako, kwani kila hali ni tofauti na inaweza kuhitaji matibabu tofauti.
 
Pia kuna aina mbalimbali za dawa zinazotumika kutibu matatizo ya tezi dume, kulingana na aina ya tatizo na kiwango cha ugonjwa. Baadhi ya dawa hizo ni pamoja na:

1. Alfa-bloka: Hizi ni dawa zinazofanya kazi kwa kupunguza shinikizo katika kibofu cha mkojo na kupunguza dalili kama vile kukojoa mara kwa mara. Mfano wa dawa hizi ni tamsulosin na alfuzosin.

2. Inhibitors ya 5-alpha reductase: Dawa hizi hufanya kazi kwa kuzuia homoni ya dihydrotestosterone (DHT) ambayo husababisha ukuaji wa tezi dume. Mfano wa dawa hizi ni finasteride na dutasteride.

3. Antibiotics: Antibiotics hutumika kutibu ugonjwa wa tezi dume unaosababishwa na maambukizi. Mfano wa antibiotics ni ciprofloxacin na trimethoprim-sulfamethoxazole.

4. Anti-inflammatory: Dawa hizi hutumika kupunguza uvimbe na maumivu katika tezi dume. Mfano wa dawa hizi ni ibuprofen na naproxen.

Ni muhimu kuzingatia kwamba matumizi ya dawa yoyote lazima yaelekezwe na daktari wako kwani kuna madhara na athari za kiafya zinazoweza kujitokeza.
 
Wakuu naomba kuelewa kwa yeyote anayejua au kushudia matibabu ya Tezi dume bila upasuaji na mgongwa kupona kabisa na hayo matibabu yanapatikana wapi?

Nitafurahi zaidi kupata taarifa za matibabu ya kisayansi kwa maana ya yanaweza kuwa wanatumia aidha dawa za asili au dawa mbadala au dawa za hospitali lakini matokeo yake yamethibitishwa kisayansi.

Natanguliza shukurani

Mim nimemtibu mtu mmoja alikuwa na tez dume amepona kabisa ,changamoto iliyopo mtu akifanyiwa upasuaji ili apone kabisa lazima akutane na daktari bingwa(specialist) maana mishipa ya tez dume imeunganika sana akikosea akaikata vibaya mtu hawez kupona maisha Yake yote na inageuka kuwa kansa na tendo la ndoa anasahau kabisa
 
Pia kuna aina mbalimbali za dawa zinazotumika kutibu matatizo ya tezi dume, kulingana na aina ya tatizo na kiwango cha ugonjwa. Baadhi ya dawa hizo ni pamoja na:

1. Alfa-bloka: Hizi ni dawa zinazofanya kazi kwa kupunguza shinikizo katika kibofu cha mkojo na kupunguza dalili kama vile kukojoa mara kwa mara. Mfano wa dawa hizi ni tamsulosin na alfuzosin.

2. Inhibitors ya 5-alpha reductase: Dawa hizi hufanya kazi kwa kuzuia homoni ya dihydrotestosterone (DHT) ambayo husababisha ukuaji wa tezi dume. Mfano wa dawa hizi ni finasteride na dutasteride.

3. Antibiotics: Antibiotics hutumika kutibu ugonjwa wa tezi dume unaosababishwa na maambukizi. Mfano wa antibiotics ni ciprofloxacin na trimethoprim-sulfamethoxazole.

4. Anti-inflammatory: Dawa hizi hutumika kupunguza uvimbe na maumivu katika tezi dume. Mfano wa dawa hizi ni ibuprofen na naproxen.

Ni muhimu kuzingatia kwamba matumizi ya dawa yoyote lazima yaelekezwe na daktari wako kwani kuna madhara na athari za kiafya zinazoweza kujitokeza.

Kumbuka hiz dawa ulizozitaja zinaondoa dalili ya ugonjwa ila hazijawahi kumtibu mtu yeyote akapona
 
Back
Top Bottom